• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Kenya ina mengi ya kujifunza kutoka sekta ya kilimo China

    (GMT+08:00) 2014-11-27 18:36:22

    Mwaka huu Kenya iliagiza magunia milioni 2.4 ya mahindi kutoka Tanzania ili kukidhi mahitaji yake ya nafaka. Lakini wakati Kenya inaponunua chakula nje, ina ardhi kubwa yenye rutuba ambayo inaweza kutosheleza kwa shughuli za kilimo kwa watu wake milioni 42. Bwana Patrick Ochola ambaye ni afisa wa kilimo kutoka Kenya na ambaye sasa anasomea shahada ya uzamili katika chuo sayansi ya kilimo cha China anaona kama serikali itawekeza fedha na pembejeo za kutosha, basi itajitosheleza kwa chakula kama vile China.

    Bw Ochola anasema kilichomchochea zaidi kuja China ni shauku ya kutaka kujifunza uzoefu wa China kuhusu usalama wa Chakula. Sekta ya kilimo katika nchi nyingi barani Afrika imepata pigo kutokana na mabadiliko ya hali ya hewa. Mwaka jana, wakulima wengi nchini Kenya walipata hasara kubwa baada ya mvua iliyoanza kunyesha msimu wa kilimo, kusababisha mafuriko makubwa ambayo yaliharibu mimea ya wakulima. Wakati huohuo, wakulima wa mahindi wa maeneo ya North Rift katika bonde la ufa na Trans Nzoia pia walipata hasara kubwa baada ya mimea yao kuambukizwa ugonjwa wasiouelewa uliobadilisha rangi ya mimea kuwa ya njano.

    Lakini baada ya kutembelea miji na mikoa mingi ili kukagua hali ya kilimo nchini China, Bw Ochola anaona hali hiyo inaweza kuepukwa kama serikali za Afrika zitashirikana na wakulima kwa karibu.

    Licha ya shirika la chakula na kilimo FAO, linapendekeza serikali kote duniani kutenga asilimia 10% ya bajeti yake kwa kilimo, Bw Ochola anaona kukosa kutimiza lengo hilo, ni moja ya sababu zinazopelekea kutojitosheleza kwa chakula.

    Bw Ochola anaona kuwa kama wanafunzi wengine wanaotaka kurudi nyumbani kusaidia juhudi za maendeleo katika nchi zao za Afrika, muhimu ni kuwasaidia wakulima wa nyumbani Kenya kupata mafanikio makubwa kwenye kilimo hususan kilimo cha biashara. Kwa kufanya hivyo, Bw Ochola anaona atakuwa amewashirikisha wakulima katika ujenzi wa taifa.

    Shirika la FAO linakadiria kuwa idadi ya watu duniani itaongezeka na kufikia bilioni 9.1 ifikapo mwaka wa 2050. Kama makadirio hayo ni kweli, basi dunia italazimika kuongeza uzalishaji wake wa chakula hadi asilimia 70. Hivi sasa macho yameelekezwa kwa serikali za Afrika kuona kama zitatimiza makubaliano ya Maputo ya kuongeza asilimia 10 ya bajeti zao kwa kilimo au la?

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako