• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Wachina wanaosoma nchi za nje watafuta fursa za ajira nchini China

    (GMT+08:00) 2014-11-27 19:33:16

    Ripoti iliyotolewa na wizara ya elimu ya China imesema, Wachina wengi wanaomaliza masomo yao nje ya nchi wanatafuta fursa za ajira nchini China. Ripoti hiyo inasema, tangu mwaka 1978 wakati China ilipotoa fursa ya masomo nje ya nchi, wachina zaidi ya milioni 3 wamefaidika na mpango huo, na mpaka kufikia mwisho wa mwaka jana, wachina milioni 1.44 walikuwa wamerudi nchini na ujuzi waliopata nje ya nchi.

    Marekani imeendelea kuwa nchi inayopendwa na wachina wanaopendelea kusomea shahada ya pili na shahada ya udaktari, huku Uingereza ikipokea zaidi wachina wanaosoma elimu ya sekondari na shahada ya kwanza.

    Ripoti hiyo inasema, karibu asilimia 50 ya wanafunzi hao wanasomea usimamizi wa biashara au uchumi, jambo linaloweza kuleta ushindani mkali nchini China.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako