• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Soko huria la jumuiya tatu za Afrika utakuza biashara kati ya China na Afrika

    (GMT+08:00) 2014-11-28 11:06:17

    Wachambuzi wanasema kwamba mpango unaopendekezwa wa kuwa na soko huria kati ya jumuiya tatu za kibiashara za Afrika utakuza zaidi biashara kati ya China na Afrika.

    Yafuatayo ni maelezo ya Ronald Mutie kuhusu mpango huo unaotarajiwa kuzinduliwa mwezi ujao nchini Misri.

    Nchi wanachama wa soko la pamoja la kusini na mashariki mwa Afrika COMESA, jumuiya ya Afrika Mashariki EAC na Jumuiya ya maendeleo ya nchi za kusini mwa Afrika SADC zinatarajiwa kuzindua mpango wa soko huru mwezi desemba.

    Litakapozinduliwa soko hilo litakuwa ndio lenya eneo kubwa zaidi la kiuchumi barani Afrika na litafungua fursa ya kubuniwa kwa soko huru la bara lote mwaka wa 2017.

    Dkt. Lubinda Habaazoka mhadhiri katika chuo kikuu cha Copperbelt nchini Zambia anasema mpango huo una fursa za kipekee za kukuza biashara kati ya China na nchi wanachama wa jumuiya hizo tatu.

    Habaazoka anasema litakapobuniwa soko hilo China itaweza kufanya mazungumzo ya kibiashara na nchi hizo kwa jumla badala ya nchi moja moja.

    Akipongeza mpango huo, Habaazoka anautaja kama uliokuja wakati unaofaa huku china ikiwa imeibuka kuwa nchi yenye uchumi mkubwa, nazo nchi za Afrika zikiendelea kushirikkiana zaidi na China ili kuongeza uwekezaji.

    Kulingana na Habaazoka kuzinduliwa kwa mpango wa soko huria kutawezehsa usafirishaji rahisi wa bidhaa na huduma lakini pia anatoa wito kwa nchi wanachama kuwa na mpango wa watu pia kusafiri bila vikwazo kwenye nchi hizo.

    Lakini huku akikaribisha mpango huo, mhadhiri huyo wa kitivo cha biashara anaonya kwamba baadhi ya viwanda huenda vikafungwa kutokana na bidhaa za bei rahisi ambazo zitaingia kwwenye soko hilo kutoka kwa nchi wanachama na hivyo anatoa wito kwa nchi hizo kuboresha uzalishaji wa bidhaa.

    Richard Musauka mkurungezi wa shiririka la kimataifa la ushirikiano wa maendeleo DPI anasema mpango huo unafanyika wakati China ikiwa imewekeza sana barani Afrika haswa kwenye miradi ya kuboresha miundo mbinu.

    Pia yeye anaoana kwamba soko huria la jumuiya tatu litakuwa na athari katika biashara kati ya China na Afrika lakini pia anatoa wito kwa China kusaidia kuleta teknolojia na kutoa mafunzo kwa watu wa jumuiya hizo.

    Soko hilo huria litajumuisha nchi 26 zenye watu milioni 625 na pato la pampoja la dola trilioni 1.2 za kimarekani hiyo ikiwa ni asilimia 58% ya pato la bara lote la Afrika.

    Kulingana na mkurugenzi wa COMESA Sindiso Ngwenya, kuzinduliwa kwa soko hilo kunafuatia mafanikio ya matakwa yaliowekwa na nchi wanachama kama vile kuongezwa ubora wa hadi asilia 75% kwa bidhaa.

    Litakapoanza soko hilo linatarajiwa kunufaisha wafanyibishara kutokana na mipango ya umoja wa forodhani na kuondolewa kwa baadhi ya vikwazo vya kibiashara.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako