• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • OPEC yadumisha kiwango cha uzalishaji wa mafuta licha ya kushuka kwa bei

    (GMT+08:00) 2014-11-28 18:32:19

    Mawaziri wa nchi wanachama wa OPEC wameamua kudumisha kiwango cha uzalishaji wa mafuta, licha ya kushuka kwa bei ya mafuta ghafi kwa kiwango kikubwa kwa mwaka wa nne mfululizo.

    Msemaji wa OPEC Hasan Hamid anasema,

    "Katika nia ya kurudisha uwiano katika soko, mkutano umeamua kudumisha uzalishaji wa mafuta wa mapipa 30 milioni kwa siku, kama ilivyokubaliwa mwezi December mwaka 2011"

    Bei ya mafuta mepesi imeshuka chini ya dola 74 kwa pipa kutokana na uamuzi huo wa OPEC, ikiwa ni kiwango cha chini zaidi tangu Septemba mwaka 2010.

    Mkutano mwingine wa nchi wanachama wa OPEC, ambazo zinazalisha asilimia 40 ya mafuta ghafi duniani, utafanyika tena mwezi June mwaka ujao.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako