• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Beijing kupiga marufuku uvutaji wa sigara ndani ya majengo ya umma

    (GMT+08:00) 2014-11-28 18:43:31

    Mamlaka ya Beijing imepitisha muswada wa kupiga marufuku uvutaji wa sigara ndani ya majengo yote ya umma, ofisi, na kwenye usafiri wa umma. Mapendekezo ya mswada huo yalipitishwa na kamati ya bunge la umma la mji wa Beijing na inatarajiwa kuanza kutekelezwa mwezi Juni mwaka ujao.

    Kulingana na mswada huo uvutaji sigara pia umepigwa marufuku kwenye maeneo ya wazi ya shule za chekechea, shule, idara zinazoshughulikia masuala ya watoto, hospitali za wanawake na watoto, maeneo ya mazoezi na michezo. Muswada huo pia unakataza kuwauzia watoto sigara kupitia mtandao wa internet pamoja na mashine.

    Matangazo ya sigara pia hayataruhusiwa barabarani, vituo vya usafiri wa umma, vyombo vya habari, vitabu, na kwenye mtandao wa internet.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako