• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Mashine za kielektroniki za kupigia kura zatumiwa kwenye uchaguzi mkuu nchini Namibia

    (GMT+08:00) 2014-11-28 19:38:52

    Namibia imekuwa nchi ya kwanza barani Afrika kutumia mashine ya kielektroniki ya kupigia kura katika uchaguzi mkuu uliofanyika leo.

    Akizungumza baada ya kupiga kura, rais Hifikepunye Pohamba amesema, anaamini kuwa teknolojia mpya imekuwa na ufanisi mkubwa zaidi kuliko taratibu nyingine.

    Teknolojia hiyo inasaidia kupunguza muda wa upigaji kura kwa siku moja. Hata hivyo vyama vya upinzani nchini humo vimeeleza wasiwasi kuhusu udanganifu unaoweza kutokea kutokana na matumizi ya teknolojia hiyo mpya na kutaka uchaguzi uahirishwe, matakwa ambayo yamekataliwa na mahakama kuu ya Windhoek.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako