• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Waziri mkuu wa China atoa wito wa kuweka mazingira mazuri ya makazi kwa wananchi

    (GMT+08:00) 2014-11-28 20:49:20

    Waziri mkuu wa China Li Keqiang amesema lengo la maendeleo ya miji ni kujenga mazingira mazuri na salama kwa watu kuishi.

    Li Keqiang amesema hayo alipotembelea maonesho ya sayansi ya makazi ya watu hapa jijini Beijing. Amesema ni lazima kuendeleza miji kwa njia ya kisayansi, na kwa wakati huohuo maendeleo hayo yasaidie maendeleo ya vijiji, ili wanavijiji nao wanufaike.

    Akizungumzia ukarabati wa sehemu ya makazi duni, Li amesema ukarabati huo unatakiwa kuharakishwa, lakini si kwa gharama ya kupoteza ubora wake.

    Ameongeza kuwa wakati watu wanapohamia sehemu za mijini, masuala ya nishati, maji, ubora wa hali ya hewa na masuala mengine ya kiikolojia yanatakiwa kufanyiwa utafiti zaidi na kutatuliwa.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako