• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Idadi ya watu walioambukizwa VVU nchini China yafikia laki 5

    (GMT+08:00) 2014-12-01 20:13:36
    Tangu kesi ya kwanza ya ugonjwa wa UKIWMI nchini China kuripotiwa mwaka 1985, idadi ya wagonjwa na watu wenye maambuziki ya UKIMWI nchini China imefikia karibu laki 5 hivi. Inafahamika kuwa, ingawa hivi sasa kasi ya maambukizi ya ugonjwa huo ni ndogo nchini China, lakini idadi ya maambukizi kwa wanafunzi vijana inaongezeka kwa kasi.

    Kauli mbiu ya Siku ya UKIMWI Duniani mwaka huu ni "kuchukua hatua, kuelekea kukomesha maambukizi ya virusi vya UKIMWI". Naibu mkurugenzi wa kamati ya taifa ya afya na uzazi wa mpango nchini China Bw. Wang Guoqiang amejulisha kuwa, hadi kufikia mwishoni mwa mwezi Oktoba mwaka huu, idadi ya wagonjwa wa ukimwi na wanaoishi na virusi nchini China imefikia laki 4.97, na watu laki 1.54 wamefariki kutokana na ugonjwa huo.

    Anasema, "Hivi sasa maambuziki ya ugonjwa wa UKIMWI nchini China yana sifa nne. Kwanza, kwa ujumla kasi ya maambukizi ya ugonjwa huo ni ndogo, lakini katika baadhi ya sehemu kasi hiyo ni kubwa. Pili, maambukizi yamepungua kwa kiwango kidogo kutokana na matumizi ya dawa za kulevya, hasa kwa kujidunga sindano kwenye mishipa ya damu, na maambukizi toka kwa mama kwenda kwa mtoto, na ngono imekuwa chanzo kuu cha maambukizi.Tatu, idadi ya watu wazima, wazee na wanafunzi vijana walioambukizwa UKIMWI inaongezeka kwa kiasi kikubwa. Na mwisho, idadi ya watu waliokufa kutokana na ukwimi imepungua."

    Miaka ya hivi karibuni, serikali ya China ilitoa sheria ya kukinga na kutibu magonjwa ya kuambukizia na kanuni za kukinga na kutibu UKIMWI, na kutoa sera mbalimbali husika, ikiwemo kupima bure virusi vya ukimwi, kutoa dawa za kupunguza makali ya ukimwi, kuzuia maambukizi ya virusi hivyo kutoka kwa mama kwenda kwa mtoto, na kuwasaidia watoto yatima ambao wazazi walifariki kutokana na ukiwmi kwenda shule na maisha yao. Hivi sasa mfumo kamili wa sheria na sera na mtandao kamili wa huduma ya kinga na matibabu ya UKIMWi umeanzishwa nchini China. 

    Habari zinasema, mpaka sasa mwanafunzi kijana mwenye umri mdogo zaidi aliyeripotiwa kuambukizwa UKIMWI nchini China ana umri wa miaka 14 tu. Mtandao wa internet unaolenga kutafuta wenzi unadhaniwa kuwa njia kuu ya kuenea kwa ugonjwa huo miongoni mwa vijana. Mkurugenzi wa kituo cha kinga na tiba ya UKIMWI katika kituo cha kinga ya magonjwa cha China Bw. Wu Zunyou anasema,

     "Tatizo la wanafunzi kuambukizwa UKIMWI linatutilia wasiwasi, idadi ya wanafunzi walioambukizwa ukimwi imeongezeka kwa kasi, wengi wao ni wanafunzi wa vyuo vikuu, hususan katika mwaka wa pili na wa tatu. Mwaka jana kulikuwa na mikoa mitano tu kote nchini iliyoripotiwa kuwa na wanafunzi 100 walioambukizwa HIV, lakini kuanzia mwezi Januari hadi Oktoba mwaka huu, idadi ya mikoa kama hiyo imefikia 10, kwa hiyo kazi ya kuwaelimisha wanafunzi kuhusu kinga na matibabu ya UKIMWI inapaswa kuimarishwa zaidi."
    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako