• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Masikilizano ya kijamii na jinsi yanavyohimizwa katika sehemu za kazi na kwenye miji mbalimbali

    (GMT+08:00) 2014-12-04 13:59:22

    Katika kipindi hiki tunazungumzia masikilizano ya kijamii na jinsi yanavyohimizwa katika sehemu za kazi na kwenye miji mbalimbali na tuangalie jambo hili lina maana gani kwenye jamii.

    Pili: China inafahamika kuwa ni nchi kubwa na yenye watu wengi. Kwa nchi kubwa na yenye watu wengi kama China, lingekuwa ni jambo la kawaida kukumbwa na changamoto na misukosuko inayotokana na migongano wakati wa maingiliano ya watu. Lakini kati hali ambayo inawashangaza wengi, China ni nchi ambayo imetulia sana. Kuna baadhi ya sehemu chache tu korofi, ambazo changamoto hutokea hapa na pale.

    Fadhili: Kuna maneno mawili ambayo ningependa hata wasilikizaji wetu wayafahamu "Masikilizano" na "uvumilivu". Mbali na kuwa makini China imeweza kuwa na utulivu kutokana na watu wake kuzingatia sana masikilizano na uvumilivu. Kuna wakati nakumbuka vyombo vya habari hapa China vilikuwa vinakumbusha mara kwa mara kuhusu masikilizano, na masikilizano na kulikuwa na mwitikio mkubwa kutoka kwa watu wa kawaida, na hata sisi wageni tukajifunza mengi.

    Pili: Moja ya mambo ninayokumbuka ni kuwa watu kwanza walikuwa wanatakiwa kuishi kwa masikilizano na watu wengine, bila kujali makabila yao, dini zao, na bila kujali kama wao ni matajiri au masikini. Tukumbuke kuwa China ni nchi yenye makabila 56, kuna pengo kubwa la maendeleo kati ya miji na vijiji, na kuna pengo kubwa kati ya matajiri na watu masikini lakini kwa ujumla China ni nchi yenye masikilizano ya hali ya juu.

    Fadhili: Kwenye nchi nyingi zenye migogoro vyanzo vinakuwa kugombea raslimali, idadi kubwa ya watu na kukosekana kwa masikilizano ya kijamii. Ukiangalia hapa China unaweza kusema ni nchi ambayo ingekuwa na migogoro lakini imetulia sana. Sababu moja kubwa ni kuwa, wachina wana jadi na utamaduni wa masikilizano na uvumilivu.

    Pili: Kuna baadhi ya mambo ambayo umetaja kuwa ni chanzo cha kutokuwepo kwa masikilizano katika jamii, maoni ambayo msikilizaji wetu Samwel Ombati wa mlimani Prison Nakuru Kenya. Msikilizaji wetu Samwel ameeleza mengi tangu ngazi ya familia, mume na mke, na hata kati ya jamii na ngazi ya taifa. Kwa hiyo tunatakiwa kukumbuka kuwa masikilizano ni kila mahali.

    Fadhili: Lakini kuna lingine la uvumilivu, hili naona ni muhimu pia. Umuhimu wake ni mkubwa zaidi katika mazingira ya sasa ambayo maingiliano ya watu wa dini, rangi, makabila na tamaduni yameongezeka sana. Hapa China tunaona wenzetu mambo haya wanafundishwa toka wakiwa watoto, kuheshimu wengine.

    Pili: Msikilizaji wetu Samwel ameeleza hayo yanayoikabili jamii ya Kenya. Lakini ukweli ni kwamba hata sisi tunafundishwa tangu tunapokuwa watoto umuhimu wa kuishi kwa masikilizano, na kweli mfano mzuri upo kwa watanzania. Wengi wamezoea kuishi kwa masikilizano kama tunavyoelezwa na msikilizaji wetu Mchana J mchana wa Morogoro Tanzania

    Fadhili: Naona hapa msikilizaji wetu anasema kuwa kwa kawaida watu huwa wanaishi kwa masikilizano wanaoleta matatizo ni wanasiasa. Hapa China wenzetu wana mfumo tofauti wa siasa ambao unaangalia maslahi ya jumla ya taifa kwanza, maslahi madogo madogo yanakuwa nyumba sana. Wenzetu wanaangalia mambo yanayohusu watu wengi wa ujumla wao.

    Pili: Inawezekana wasikilizaji wetu wanajiuliza ni kwanini nchi kubwa kama China yenye watu wengi imetulia, wakati ina idadi kubwa ya watu na makabila. Ua watu huwa hawakorofishani? Kama kuna wasikilizaji watakuwa wamebahatika kuona ile tamthuiliya ya Doudou na mama wakwe zake watakuwa wanajua kuwa mikwaruzano inatokea, lakini wenzetu wana uvumilivu na kuangalia maslahi makuu ya pamoja na sio ya mtu mmoja mmoja.

    Fadhili: Lakini kuna lingine ambalo tumelizungumza mwanzo, kuwa masilikizano sio kati ya watu na watu peke yao, bali ni watu pamoja na mazingira wanayoishi. Kwa sasa ukiangalia hapa China wenzetu wana kampeni kubwa sana za kuhifadhi mazingira, ingawa tunaona hewa inachafuka kutokana na vinwada na moshi wa magari, lakini upandaji wa miti, kuzia jangwa na hata shughuli nyingine za kulinda mazingira zinafanyika sana ili watu wawe na maisha bora.

    Pili: hili huwa pia linawafurahisha wageni wengi wanaokuja hapa China kwa ziara fupi fupi, hasa pale wanapoonza kando ya barabara kuna miti, kwenye makazi ya watu kuna bustani na hata kwenye baadhi ya maeneo ya kiofisi kuna sehemu za kijani. Na la kushangaza ni kuwa mazingira ya Beijing ni magumu sana kwa mimea kukua. Ikija baridi majani yote yanaungua na miti inakaribia kufa, lakini yakiingia majira ya joto wanajitahidi sana kuhakikisha wanayarudisha katika hali ya kawaida. Ina maana wenzetu sio tu wanajali maisha yao hata pia ya mimea yao.

    Fadhili: Hili ni moja kati ya mambo ambao wasikilizaji wetu wanayazungumzia mara kwa mara kama anayoeleza msikilizaji wetu mchana J mchana.

    Pili: Naona msikilijzia wetu Mchana J Mchana analia na viongozi, yeye anana viongozi wanatakiwa kuongoza kwa mfano. Kama wanazungumzia masikilizajo basio wasiwe chanzo cha uchochezi, na kama wanazungumzia kulinda mazingira basi wao ndio wawe wa kwanza.

    Fadhil: Ni kweli viongozi wanatakiwa kuonesha mfano, lakini hata sisi wenyewe tusirubuniwe tu kirahisi ay kuwabebesha mzigo viongozi bila sisi kuitekeleza wajibu wetu.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako