• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Siangaliii jinsia yangu ninapocheza muziki; asema DJ wa kike kutoka Afrika mjini Beijing China

    (GMT+08:00) 2014-12-10 13:45:37

    Kazi ya DJ mara nyingi inachukuliwa kuwa ya wanaume.
    Lakini aghalabu kwenye karne hii ya 21 wanawake wameanza kuonyesha ubabe wao kwenye kazi hiyo ya burudani.
    Hivi leo mwandishi wetu Ronald Mutie amekutana na Rachael Wamoto ama kwa jina lake la kazi DJ Miss Ray ambaye mbali na kusomea kazi ya utengenezaji filamu pia ni DJ mjini Beijing.


    Rachael Wamoto ama kwa jina lake la kazi DJ Miss Ray ambaye mbali na kusomea kazi ya utengenezaji filamu pia ni DJ mjini Beijing. Anatumbuiza watu kwenye klabu moja maarufu mjini akicheza sana nyimbo za kiafrika.

    DJ Miss Ray kwanza alikumbana na changamoto ya kujenga umaarufu kwa sababu watu wengi hawajazoea kuona DJ wa kike na zaidi kuona DJ wa Afrika kwenye sehemu za burudani za China. Lakini kwa sasa anasema watu wengi wamemjua na anavutia sio waafrika tu lakini watu kutoka nchi mbali mbali.

    DJ Miss Ray anasema muziki wa Afrika unaopendendwa na wenfgi ni wa kutoka Nigeria. Lakini hata hivyo akiwa DJ anajaribu kucheza miziki kutoka maeneo mbalimbali ili kuridisha mashabiki wake wote. Kama njia ya kuendeleza kazi ya DJ wa Afrika wamefungua ukurasa kwenye mitandao ya kijamii ambapo wanawasilinana.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako