• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Wakati umefika kwa China kuchukua nafasi kwenye hali mpya ya kawaida.

    (GMT+08:00) 2014-12-17 09:52:13

    Katika mji wa Linshui, wenye watu wa makabila madogo kisiwani Hainan China, sekta ya ujenzi wa nyumba imekuwa ikihimiza ukuaji wa kiuchumi kwa muongo mmoja uliopita. Lakini mwaka huu hali imekuwa tofauti na uwezo wa sekta hiyo umepungua kiasi. Mauzo ya eneo la jumla la nyumba yalipungua kwa asilimia 14.7, na mauzo ya nyumba yalipungua kwa asilimia 7.4 katika miezi tisa ya kwanza ya mwaka huu na hivyo kuifanya serikali ya mji huo kuangalia upya sera yake ya maendeleo ya kiuchumi.

    Mkuu wa serikali za mitaa Bw Yang Wenping, alisema walihisi mabadiliko katika soko na uchumi kwa ujumla, hali ambayo inaitwa "mpya ya kawaida"' na kwamba wanajua ili kuleta ustawi, wanapaswa kubadili njia ya maendeleo ya kiuchumi na kutafuta mbinu mpya za kuendesha uchumi wao. Mji huo umetafuta ushirikiano na nchi nyingine kama vile Singapore, Israel na makampuni ya kimataifa kama Microsoft kuleta teknolojia ya kisasa na uwekezaji kwenye sekta ya kilimo utafiti na teknolojia ya habari.

    Na juhudi za mji huo mdogo za kuzoea "hali mpya ya kawaida" zimefungua fursa kote duniani na hiyo ni sambamba na mwongozo wa mkutano muhimu wa kiuchumi wa chama cha kikomunisti cha China CPC, uliokamilika wiki hii.

    Kwenye mkutano huo, viongozi wa China walieleza sera kuu za kiuchumi na maswala yatakayopewa kipaumbele mwaka kesho, ambayo sio tu yanatarajiwa kuinufaika China, bali dunia nzima. Kwa mujibu mkutano huo, China itaufanyia marekebisho muundo wake wa biashara na uwekezaji ili kufikia urari wa malipo ya kimataifa. Pia muundo huo utapanua soko katika sekta ya huduma, kufungua zaidi sekta ya viwanda, na kukuza mapango wa majaribio wa eneo la soko huria la China-Shanghai(FTZ).

    Ifikapo mwaka wa 2020, idadi ya watu wenye mapato ya wastani nchini China itafikia milioni 600, kiwango cha uagiziaji wa bidhaa kutoka nje kuwa zaidi ya dola trilioni 17 za kimarekani huku nao uwekezaji wa China nchi za nje ukifikia dola trilioni 1.2 za kimarekani.

    Kwa mujibu wa katibu mkuu wa kamati ya kitaaluma katika Tume ya Taifa ya Maendeleo na Mageuzi Bw. Zhang Yansheng, ongezeko hilo la biashara na uwekezaji lina maana kwamba kutakuwa na ajira mpya milioni 7 na ukuaji wa asilimia 27% wa Pato la Taifa kote duniani. Bw Zhang pia amesema mapato ya watu wa China yakiongezeka, wananchi watakuwa na hamu zaidi ya kununua bidhaa bora za kimataifa, na hivyo sera za kuuza nje na kuagiza zinatarajiwa kubadilishwa kulingana na hali ilivyo.

    Mchumi wa shirika la Goldman Sachs Bw Ha Jiming anasema kubadilikla kwa mahitaji ya bidhaa kwa wachina, kunamaanisha sasa ni wakati wa kubadilisha jinsi ya kutengeneza bidhaa kutoka hali ya sasa ya kutengenezea china hadi ile ya kutengeneza "Kwa ajili ya China." Anasema mahitaji ya chakula salama, magari, huduma za fedha na kusafiri nje ya nchi kunatarajiwa kukua kwa kasi na kwa kiwango kikubwa.

    China ambayo kwa sasa inakabiliwa na shinikizo la kuboresha viwanda na urekebishaji wa uchumi, inazidi kutafuta soko la nje. Makampuni ambayo yamekuwa yakitegemea ukuaji wa haraka wa China kwa ajili ya soko ya bidhaa zao kwa zaidi ya miongo mitatu sasa, yataanza kutafuta masoko mapya.

    Uwekezaji wa moja kwa moja wa China nje ya nchi yaani ODI unatarajiwa kuupiku uwekezaji wa kigeni wa moja kwa moja yaani FDI kwa mara ya kwanza mwaka huu. Karibu makampuni 5,000 ya Kichina yamewekeza kwenye nchi na maeneo 154 katika miezi kumi ya mwanzo ya mwaka huu. Uwekezaji wa moja kwa moja wa China nje ya nchi ODI wa makampuni yasiyo ya kifedha uliongezeka kwa asilimia 17.8% na kufikia dola bilioni 81 za marekani.

    Kwa mujibu wa wizara ya biashara, wakati huo huo uwekezaji wa kigeni wa moja kwa moja yaani FDI nchini China ulishuka kwa asilimia 1.2% na kufikia dola za kimarekani bilioni 96.

    Mkuu wa kitivo cha elimu ya Masuala ya Kimataifa na Umma ya Chuo Kikuu cha Columbia Merit E. Janow anasema makampuni ya Kichina ambayo yanawekeza nje ya nchi sasa yameanza kuwekeza kwenye sekta mpya kama teknolojia na bidhaa, mbali na sekta za jadi za maliasili. Pia amesema juhudi za China za kuwezesha uvumbuzi na kukua kwa miji pamoja na kuendeleza sekta ya huduma ya kisasa zinahitaji uzoefu wa kimataifa na ushirikiano. China pia inahimiza uwazi kwenye uchumi wa dunia kwa kujenga mitandao ya mshikamano wa biashara ya kikanda na kuimarisha uhusiano.

    Majukwaa ya kikanda ya ushirikiano wa kiuchumi kama vile Benki ya uwekezaji wa miundo mbinu ya Asia, benki ya maendeleo ya nchi za BRICS, mfuko wa barabara ya Hariri na mradi wa treni ya kasi ya Asia na Ulaya yatasaidia kuhumiza ushirikiano wa kikanda.

    China imesaini mikataba 12 ya biashara huria na kupunguza vikwazo vya biashara katika nchi na maeneo 20 kwa ajili ya kuhimiza biashara. China pia imekamilisha mazungumzo ya biashara huria kati yake na Korea Kusini na Australia.

    Bwana Zhang anasema juhudi za China kukubaliana na "hali mpya ya kawaida" haimaanishi tu kufuata mfano wa kuboresha ukuaji wa uchumi, lakini pia inaweza kuchangia zaidi kuwa na mfumo wazi wa maendeleo na ufanisi wa kikanda na kimataifa.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako