• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Wachumi wakuu wachambua mkutano wa kamati kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China kuhusu kazi ya uchumi

    (GMT+08:00) 2014-12-17 09:52:58

    Mkutano wa kamati kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China uliofungwa hivi karibuni ulithibitisha mwelekeo wa sera ya uchumi, majukumu ya kazi ya uchumi na malengo ya maendeleo katika mwaka 2015. Mkutano huo umeeleza mabadiliko sita mapya ya maendeleo ya uchumi katika hali mpya ya kawaida.

    Ukiwa mkutano unaoamua sera ya uchumi nchini China, mkutano huo umefanyika wakati kasi ya ongezeko la uchumi inapopungua na maendeleo ya uchumi yameingia kwenye hali mpya ya kawaida, hivyo mkutano huo umefuatiliwa sana na soko la nje na ndani. Wachumi wakuu wengi wa benki maarufu za uwekezaji wametoa maoni mbalimbali kuhusu mkutano huo.

    Mchumi mkuu wa Benki ya Uswisi nchini China Bw. Wang Tao amesema, viongozi wa China wameeleza kwa makini hali mpya ya kawaida katika nguvukazi, mahitaji kutoka nje na vizuizi kwa mujibu wa maliasili na mazingira, hii inaonesha kuwa serikali ya China itaweka lengo la ongezeko la uchumi la mwaka kesho kwenye kiwango cha chini kidogo, pia haitachukua sera za kuhamasisha uchumi kwa pande zote.

    Bw. Wang Tao ameona kuwa kutokana na kukabiliana na shinikizo kubwa la kudidimia kwa uchumi, kudumisha ongezeko la uchumi kwa utulivu kumewekwa na serikali ya China kuwa jukumu la kwanza la majukumu tano ya kazi ya uchumi mwaka 2015, hii itaweka mazingira ya utulivu kwa kufanya mageuzi na kupunguza hatari ya mfumo. Na taarifa iliyotolewa na mkutano wa kamati kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China imetangaza kuwa China itaharakisha mageuzi ya maeneo tisa ikiwemo ukaguzi wa kiserikali, uwekezaji na bei, hali hii inatarajiwa kusaidia kutokea kwa ongezeko jipya la uchumi.

    Mkutano huo umesema, maendeleo ya uchumi wa China yameingia kwenye hali mpya ya kawaida, uchumi wa China unaongezeka kwa kasi ya kati na kubwa kutoka kasi kubwa. Mchumi mkuu wa kampuni ya fedha ya China Bi. Liang Hong amesema, ni lazima kudumisha ongezeko la kasi ya kati na kubwa, pia lengo hilo linaweza kutimizwa. Anaona kuwa kutokana na upande wa ajira, ni lazima kudumisha ongezeko la asilimia 7 hadi 7.5.

    Mchumi mkuu wa Benki ya HSBC Bw. Qu Hongbin ameona kuwa, kati ya majukumu matano yaliyotolewa na mkutano wa kamati kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China, kudumisha ongezeko la uchumi kwa utulivu na kuhimiza mageuzi bado ni majukumu yanayopewa kipaumbele. Taarifa ya mkutano imeeleza umuhimu wa mabadiliko ya majukumu na uwezo wa serikali, hii inaonesha kuwa mwaka kesho mageuzi ya serikali yataimarishwa. Na kampuni za kitaifa zitazingatia kuinua ufanisi na kupanua uwekezaji kwa nje.

    Bw. Qu Hongbin amesema, kama kawaida, taarifa ya mkutano wa mwaka huu haitaji lengo la makini la ongezeko la uchumi wa China. Ameona kuwa lengo hilo huenda litapangwa kuwa kati ya asilimia 7 hadi 7.5.

    Mchumi mkuu wa Benki ya Uswisi Bw. Wang Tao amesema, taarifa hiyo inasema China itatimiza uwiano kati ya mapato na utoaji wa kimataifa hatua kwa hatua, hii inamaanisha kuwa serikali ya China itatumia fursa ya kupungua kwa bei ya mafuta, na kuongeza idadi ya mafuta yanayoagizwa, vilevile itaongeza uagizaji wa bidhaa na huduma nyingine, ili kuzuia kuinua kwa urari wa biashara. Bw. Wang Tao pia anatarajia kuwa serikali ya China itahimiza uwekezaji nje, na kuziunga mkono kampuni za China kuwekeza katika nchi nyingine kwa kupitia mpango wa ujenzi wa eneo la uchumi la njia ya hariri. Pia anaona kuwa China itaongeza mahitaji ya nje ya bidhaa za China, wakati huo huo itazuia ongezeko la akiba za fedha za kigeni.

    Mchumi mkuu wa kampuni ya fedha ya China Bi. Liang Hong pia ameona kuwa kuwekeza nchi za nje kumekuwa mkakati wa kitaifa wa China. Baada ya kudumisha urari mzuri wa biashara kwa miaka 20, China imeingia kwenye kipindi cha kuongeza uwekezaji nje kwa kiasi kikubwa. Bi. Liang Hong amesema kupanua uwekezaji nje si kama tu ni pamoja na ujenzi wa miundo mbinu, mashine za ujenzi wa miradi, bali pia kunahusu pia aina mbalimbali za uwekezaji wa akiba za fedha za kigeni na kuanza kutumika kwa sarafu ya China RENMINBI kimataifa, na kupanua fursa ya eneo la kifedha kwenye kupata maendeleo nje ya nchi.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako