• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Li Keqiang ahudhuria kongamano la uchumi na biashara kati ya China na CEE

    (GMT+08:00) 2014-12-17 11:15:43

    Waziri mkuu wa China Bw. Li Keqiang amehudhuria na kutoa hotuba kwenye ufunguzi wa mkutano wa nne wa Baraza la uchumi na biashara kati ya China na nchi za Ulaya ya kati na mashariki huko Belgrade, Serbia.

    Bw. Li amesema ufufukaji wa uchumi duniani ni dhaifu, na nchi nyingi zinakabiliwa na shinikizo la kuzorota kwa uchumi, hivyo jukumu la kudumisha ongezeko la uchumi ni gumu. Amesema pengo la kimaendeleo lililokuwepo nchini China na katika nchi za Ulaya ya kati na mashariki hata nchi nyingine duniani linaleta fursa kubwa ya maendeleo.

    Bw. Li ameongeza kuwa kuongeza ushirikiano kati ya China na nchi za Ulaya ya kati na mashariki kwenye msingi wa utaratibu na sheria za Umoja wa Ulaya kutasaidia kuleta usawa wa maendeleo barani Ulaya, na kuzinufaisha pande zote mbili.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako