• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Rais wa China atoa salamu za rambirambi kufuatia shambulizi la kigaidi lililotokea jana nchini humo

    (GMT+08:00) 2014-12-17 19:45:27
    Rais Xi Jinping wa China ametoa salamu za rambirambi kwa mwenzake wa Pakistan Mamnoon Hussain kufuatia shambulizi la kigaidi lililotokea jana kwenye shule inayoendeshwa na jeshi katika jimbo la Peshawar na kusababisha vifo vya watu 141.

    Katika salamu zake, rais Xi amesisitiza kuwa, China inapinga aina zote za ugaidi na kulaani vikali shambulizi hilo. Ameongeza kuwa nchi yake inaunga mkono kithabiti jitahida zinazochukuliwa na serikali ya Pakistan katika kupambana na ugaidi.

    Wakati huohuo, waziri mkuu wa China Bw. Li Keqiang naye pia ametoa salamu za rambirambi kwa mwenzake wa Pakistan Bw. Nawaz Sharif.

    Na  Pakistan leo imeanza siku tatu za maombolezo kwa vifo vya watu 145 vilivyotokana na shambulizi hilo na kutangaza kurejesha adhabu ya kifo kwa wahalifu wa kigaidi.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako