• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Rais wa Marekani kusaini mswada wa kuongeza vikwazo dhidi ya Russia

    (GMT+08:00) 2014-12-17 19:46:41

    Ikulu ya Marekani imesema rais Barack Obama anatarajiwa kusaini mswada wa sheria uliopitishwa na bunge kuhusu kuongeza vikwazo dhidi ya Russia na kutoa misaada ya ziada kwa Ukraine.

    Kwa mujibu wa mswada huo, Marekani itakubali Ukraine, Georgia na Moldova kuwa washirika wake mbali na Jumuiya ya Kujihami ya NATO, kuweka vikwazo vipya dhidi ya makampuni makubwa ya Russia, na kutoa msaada wa kijeshi wenye thamani ya dola za Marekani milioni 350 kwa Ukraine, yakiwemo makombora ya kushambulia vifaru.

    Wakati huohuo, Wizara ya Mambo ya Nje ya Russia imesema, nchi hiyo itajibu vikwazo hivyo itakayowekewa na Marekani.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako