• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Serikali ipunguze bei ya nishati na gesi

    (GMT+08:00) 2014-12-17 19:56:19
    Kaimu katibu wa Mkoa wa Pwani, Shangwe Twalama anasema Serikali inapaswa kuweka utaratibu wa kupunguza bei ya gesi ili wananchi waendelee kununua.

    Bi:Twalama anasema hayo katika warsha iliyoandaliwa na mtandao wa nishati.

    Aidha alisema utaratibu huo utasaidia kukabiliana na uharibifu wa mazingira unaotokana na ukataji wa miti kwa ajili ya mkaa na kuni.

    Bi;Twalama anasema asilimia kubwa ya wananchi wanashindwa nunua gesi kwa ajili ya bei ya juu, badala yake wanakimbilia mkaa na kuni, jambo linalosababisha jangwa.

    Mwanachama wa mtandao Gisela anasema endapo halmashauri zitashirikiana vizuri na wadau pamoja na mashirika yanayojihusisha na utafiti wa uzalishaji wa nishati kwa njia mbalimbali, itakuwa rahisi kufikia malengo husika.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako