• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Ondoeni VAT kwa ajili ya kukuza biashara.

    (GMT+08:00) 2014-12-17 19:57:03

    Wataalam wa kibiashara nchini Rwanda wameitaka serikali ya nchi hiyo kuondoa kodi ya thamani katika bidhaa zinazouzwa nje kama njia moja ya kukuza biashara hiyi nchini Rwanda.

    Mkurugenzi mkuu wa wataalam hao nchini humo David Primack anasema sekta hiyo ya kibiashara ya nje ya nchi, nchini Rwanda imekuwa ikifanya vyema lakini kama serikali inataka ifanye vyema zaidi inafaa kuondoa kodi hiyo ya thamani.

    Aidha anasema bidhaa za Rwanda zikiondolewa kodi ya thamani zitakuwa na soko zaidi Kimataifa ikilinganishwa na bidhaa kutoka mataifa yaliyo na bidhaa zilizo na kodi hiyo.

    Pia, wataalam hao wameitaka serikali ya nchi hiyo kuchukua fursa ya kuwapa mafunzo ya kibiashara wanabiashara wa nchi hiyo ili kuchangamkia biashara ya Kimataifa vilivyo kama wenzao kutoka mataifa jirani ya kanda.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako