• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • China yasema Umoja wa Mataifa unapaswa kuunga mkono juhudi za Umoja wa Afrika katika kulinda amani

    (GMT+08:00) 2014-12-17 20:08:43
    Mjumbe wa kudumu wa China kwenye Umoja wa Mataifa Bw. Liu Jieyi amesema, Umoja huo unapaswa kuheshimu matakwa ya Afrika, na kuunga mkono juhudi za Umoja wa Afrika za kulinda amani katika kutatua migogoro ya kikanda barani Afrika.

    Bw. Liu Jieyi amesema hayo kwenye mkutano wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kuhusu ushirikiano kati ya umoja huo na Umoja wa Afrika katika operesheni za kulinda amani. Bw. Liu amesema, Umoja wa Afrika una uelewa na ufahamu zaidi kuhusu suala la kutatua masuala yaliyopo barani Afrika, na unaweza kutoa ufumbuzi wa masuala hayo kwa mtazamo wa Afrika yenyewe, hivyo Baraza la Usalama linapaswa kuweka kipaumbele katika kuunga mkono kazi muhimu za Umoja wa Afrika kutatua migogoro ya kikanda, na kusikiliza maoni na mapendekezo ya Umoja wa Afrika.

    Bw. Liu Jieyi ameongeza kuwa, ushirikiano thabiti kati ya Umoja wa Mataifa na Umoja wa Afrika unahitajika kwa ajili ya kuendeleza ushirikiano wa kimataifa na kwa maendeleo ya mfumo wa kimataifa wa usalama wa pamoja.
    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako