• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Mtu mmoja afariki na wengine 6 kujeruhiwa baada ya jengo kuporomoka mjini Nairobi

    (GMT+08:00) 2014-12-17 20:16:57

    Mtu mmoja amefariki dunia na wengine sita kujeruhiwa, baada ya  jengo moja kuporomoka mjini Nairobi.

    Imefahamika kuwa, jengo hilo lenye ghorofa tano ambalo bado linaendelea kujengwa liliporomoka saa tisa alfajiri ya leo. Katibu mkuu wa wizara ya mipango na ugatuzi Bw. Peter Mangiti amesema, kazi za kuwaokoa wale walionasa kwenye vifusi zinaendelea. Naye naibu gavana wa kaunti ya Nairobi Bw. Jonathan Mueke ameeleza kuwa wanamsaka mwenye jengo hilo, ambalo umiliki wake bado haujathibitishwa, na kwamba imefahamika kuwa mwenye jengo hilo hakupata vibali vya kumiliki jengo hilo.
    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako