• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Benki ya Dunia kuongeza mkopo wa dola milioni 75 za kimarekani kwa ajili ya ukarabati wa Bwawa la Kariba

    (GMT+08:00) 2014-12-17 20:29:28

    Benki ya Dunia leo imeongeza mkopo wa masharti nafuu wa dola milioni 75 za kimarekani kwa Zimbabwe na Zambia kwa ajili ya ukarakabati wa Bwawa la Kariba linalotumiwa kwa pamoja na nchi hizo jirani.

    Bwawa hilo lililojengwa katika miaka ya 60 ni kituo cha pili kwa ukubwa cha kuzalisha umeme nchini Zimbwabwe, kinachotoa umeme megawati 700.

    Akiongea kwenye mkutano na waandishi wa habari, mkurugenzi wa Benki ya Dunia nchini Malawi, Zambia na Zimbabwe, Kundhavi Kadiresan amesema Benki ya Maendeleo ya Afrika kwa upande wake itatoa mkopo wa dola milioni 75, huku Umoja wa Ulaya ukitoa dola 100 na Sweden itatoa dola milioni 25 ili kusaidia mradi huo utakaogharimu jumla ya dola milioni 295 za kimarekani.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako