• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Hakuna watu wenye msimamo mkali na wasio na msimamo mkali ndani ya chama na serikali ya China katika suala linalohusu Tibet

    (GMT+08:00) 2014-12-17 21:09:24

    Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya China Bw. Qin Gang amesema, Dalai Lama anatakiwa kuacha nia yake ya kuitenganisha Tibet kutoka China, na kuchukua hatua ya kuweka mazingira kwa ajili ya kuwasiliana na serikali kuu ya China.

    Kauli ya msemaji huyo inatokana na habari kuwa, hivi karibuni Dalai Lama alipohojiwa na televisheni ya Ufaransa alisema anaona kuwa, ndani ya serikali kuu ya China, kuna watu wasio na msimamo mkali na pia wenye msimamo mkali katika kujadili hatma ya mkoa wa Tibet na suala la "kujitawala" kwa mkoa huo.

    Bw. Qin Gang amesema katika suala la Tibet, hakuna watu wenye msimamo mkali au wasio na msimamo mkali ndani ya Chama cha kikomunisti cha China na serikali ya China, na kupinga ufarakishaji wa taifa, kulinda umoja wa kitaifa na ukamilifu wa ardhi, na kulinda umoja wa makabila ni nia imara ya watu wote wa China.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako