• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Marekani na Cuba zachukua hatua za kurejesha uhusiano wa kawaida

    (GMT+08:00) 2014-12-18 10:13:11

    Rais Barack Obama wa Marekani ametangaza sera mpya kwa Cuba, ikiwa ni moja ya hatua za kurejesha uhusiano wa kawaida na kukomesha hali ya kutengana kati ya nchi hizo mbili iliyodumu kwa miongo mitano.

    Rais Obama amemtaka waziri wa mambo ya nje Bw. John Kerry kuanzisha mazungumzo na Cuba kuhusu kurejesha uhusiano wa kibalozi kati yake na Cuba, uliositishwa Januari mwaka 1961 kutokana na Marekani kuitaja Cuba kuwa nchi inayofadhili ugaidi. Rais Obama ameongeza kuwa Marekani itarejesha ubalozi huko Havana, mji mkuu wa Cuba na kufanya ziara ya ngazi ya juu nchini humo.

    Taarifa hiyo imetolewa baada ya rais Obama kuzungumza kwa njia ya simu na rais Raul Castro wa Cuba. Hii ni mara ya kwanza kwa viongozi wa nchi hizo mbili kufanya mawasiliano ya moja kwa moja katika muda wa zaidi ya miongo mitano iliyopita.

    Mapema siku hiyo Cuba iliwaachia huru mmarekani Alan Gross na jasusi mmoja wa Marekani waliokuwa wanashikiliwa kwa miaka mitano na 20 mtawalia.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako