• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Karamu na mikutano inaleta mshikamo miongoni mwa wanafunzi waafrika mjini Beijing

    (GMT+08:00) 2015-01-15 16:07:45

     

    1. Wananfunzi wakipakua chakula wakati ya karamu ya kufunga mwaka 2014 kwenye Chuo kimoja hapa Beijing. Wanafunzi wa Kenya wameunda chama chao na wanakutana mara moja kwa mwezi kubadilishanana maoni na kuzungumzia maswala ya elimu na mengine yanayohusu maisha ya kila siku.

    2. Purity Kabibi na Jacqueline Makena walisaida kuandaa chakula siku ya karamu. Wanasema mkutano na karamu kama hii inawafanya wahisi kama wako nyumbani haswa baada ya mwezi mzima darasani. Hawa ni miongoni mwa zaidi ya wanafunzi 2,000 wa Afrika wanaosomea nchini China wengi wao wakiwa chini ya mpango wa msaada wa masomo wa serikali ya China.

     

    Kila mwaka serikali ya China inatoa msaada wa masomo kwa mamia ya wanafunzi wa Afrika kuja kusomea China.

    Hii inamaanisha wengi wao watakaa mbali na nyumbani ama familia kwa muda mrefu.

    Lakini ili kujiweka katika hali ya jamii baadhi yao wanaunda vikundi na kuandaa mikutano mara kwa mara na kubadilishana mawazo kuhusu masomo na hali ya maisha.

    Ronald Mutie alikutana na mojawepo wa vikundi vya wanafunzi hapa beijing.

    Ni maombi kabla ya kuanza karamu ya kufunga mwaka 2014 kwenye Chuo kimoja hapa Beijing.

    Wengi wa wanafunzi kwenye karamu hii ni waafrika kama Purity Kabibi kutoka Kenya.

    "Inanifanya nahisi kama niko nyumbani na nafurahi kuungana na wenzangu. Ukitoka nyumbani na kuja sehemu ambayo hakuna watu wa kwenu unajiskia mpweke lakini ukipata marafiki wanakualika mahali kama hapa unajiskia uko nyumbani"

    Lakini leo pia kuna baadhi ya wengine kutoka nchi kama vile Russia na Pakistan.

    Solomon Omwoma ndiye mwenyeji na mwandalizi wa karamu ya leo na amekuwa akipika vyakula vya kiafrika mchana kutwa.

    "Katika hali ya kufurahia tumeamua tuje pamoja, tusherehekee na tufurahie kama wakenya walioko nje na tukiwa hapa China hatujulikani kama wakenya tunajikusanya pamoja na kuwa waafrika ndio maana umepata wa Ethiopia na wa Ghana "

     

    1. Solomon Omwoma kutoka Kenya akiwa kwenye chuo chake mjini Beijig. Amewaandalia wanafunzi wa Afrika karamu. Wanafunzi wa Kenya Mjini Beijing kwa mfano walianzisha shirikisho mwaka wa 2006 ili kukuza mshikamo miongoni mwao. Anasema karamu hii inawasaidia kukumbukana hata miaka mingi baada ya kukamilisha masomo yao Beijing.

    2. Beatrice Maisori, katibu wa shirikisho la wanafunzi wa Kenya mjini Beijing, China anasema linawasaidia wanafuzni kuzoea maisha mapya wanachama wanakutana kupanga safari kuzuru maeneo mbalimbali nchini China. Kila mwaka zaidi ya wanafunzi 200 kutoka Kenya hujiunga na vyuo mbalimbali nchini China.

     

    Kuna vyakula kama vile Ugali, samaki, mboga na vinyaji mbali mbali na zaidi ya wanafunzi mia moja wanahudhuria karamu ya leo.

    Jacqueline Makena leo pia amekuwa jikoni kusaidia kuandaa Chakula.

    "Nimetengeneza mchuzi wa viazi na kuandaa meza na pia kupika chai. Nina furaha kuja hapa kuona wakenya wenzangu na watu wengine na naona ni kitu muhimu kwa sababu ukikaa darasani na kusoma peke yako na wakati mwingine vitu ni ngumu unapata kuna shinikizo nyingi lakini ukija hapa ni kama nyumbani"

    Wanafunzi wa nchi za Afrika wanaosomea Beijing wameunda vikundi ambavyo huwakutanisha mara kwa mara

    Wanafunzi wa Kenya Mjini Beijing kwa mfano walianzisha shirikisho mwaka wa 2006 ili kukuza mshikamo miongoni mwao na wanakutana kila jumapili ya kwanza ya mwezi katika maeneo mbalimbali.

    Beatrice Maisori, katibu wa shirikisho hilo anasema linawasaidia wanafuzni kuzoea maisha mapya.

    Pia wanachama wa shirikisho hili wanakutana na kupanga safari kuzuru maeneo mbalimbali nchini China

    "Tunakutana ili tuweze kusaidia yeyote mwenye ako na shida yoyote kama kwa shule ama kununua vitu madukani. Pia kuna wakati tumekuwa na wenye wamefiwa na jamaa zao na jambo kama hilo likitokea mtu atahitaji kusafiri kwenda kuungana na familia yake, kwa hivyo tunaangalia ni vipi tunaweza kumsaidia. Na pia wakati wa sherehe za kufuzu tunakuja pamoja na kushrehekea kwa sababu jamaa za wanachama wetu wako mbali"

    Kila mwaka zaidi ya wanafunzi 200 kutoka Kenya hujiunga na vyuo mbalimbali nchini China ikiwa ni sehemu ya mpango wa serikali ya China wa kutoka msaada wa masomo kwa wanafunzi wa Afrika.

    Na huku China ikiendelea kuwa mojawepo wa nchi ambayo wanafunzi wanachagua kuendeleza masomo yao, chama hiki cha wanafunzi kitakuwa na wanachama zaidi siku za baadaye.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako