• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Wataalam wa kisayansi wahimiza utafiti na uongozi ili kukabili ebola

    (GMT+08:00) 2015-01-16 10:06:53

    Wataalam wa sayansi waliokutana mjini Nairobi Kenya wamesema ili kufanikiwa kwenye vita dhidi ya ebola, nchi za Afrika zitahitaji mipango ya kimkakati kama vile utafiti wa tiba, nguvu kazi na uongozi bora.

    Walisema Ebola inaendelea kuwa changamoto kubwa kwa afya na inahitaji kushugulikiwa kwenye ngazi ya kitaifa na kikanda.

    Profesa Vinicent Titanji kutoka taasisi ya sayansi ya Afrika alisema kutokea kwa ebola Afrika Magharibi kunatoa mafunzo ya jinsi ya kuwekeza kwenye hatua kama vile tahadhari za mapema, uongozi na kuelimisha jamii. Pia amesema Ebola imefungua ukurasa wa mjadala mpya wa jinsi ya kukabiliana na maradhi ya kuambukiza.

    Takwimu za mwezi huu kutoka shirika la afya duniani WHO zimeonyesha kwamba zaidi ya watu 20, 700 wameambukizwa maradhi hayo na 8, 200 tayari wamefariki dunia nchini Guinea, Liberia na Sierra Leone.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako