• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Nilihofia maisha magumu na mwanangu Beijing lakini sasa nafurahi anaongea kichina vizuri

    (GMT+08:00) 2015-01-16 15:16:08

    Beatrice Maisori alikuja China kwa masomo zaidi mwaka wa 2013.

    Ikiwa ni mara yake ya kwanza kuja China alikuwa na maswali mengi ya kujibu kuhusu vile atakavyoishi kwenye nchi ambayo lugha na tamaduni zake ni tofauti sana na zile za Afrika na hususan Kenya.

    "Siku ya kwanza tu nilipofika uwanja wa ndege nilipata kila mtu anaonmgea kichina wala hakukuwa na kiingereza."

    Wiki ya kwanza akiwa Beijing Beatrice alianza kujifunza lugha ya kichina na ingawaje haikuwa rahisi alijikakamua na sasa anaweza kuwasiliana vyema.

    Lakini hiyo haikuwa ndio tatizo la pekee kwa Beatrice.

    Kabla ya kuondoka nyumbani alikabiliwa na kitendawili kingine.

    Aliitaji kusafiri na mwanawe Tephilla mwenye umri wa miaka 10 kwani alifahamu fika kwamba akiwa mbali naye hataweza kuwa makini na masomo yake na atahitaji kusafiri mara nyingi kurudi Kenya kwa ajili ya mwanawe.

    "Haikuwa rahisi kufikiria vile nitaenda na mtoto kwa sababu China ni nchi ya kigeni na sijawahi kuja China tena na sikujua vile nitaishi na yeye na wenye niliwauliza waliniambia mfumo wa masomo ni tofauti kabisa na ile ya nyumbani"

    Betreace alikata kauli kwamba hata kama itabidi awe mwalimu wa mtoto wake atafanya hivyo.

    Alivalia njuga na kuamua kupambana na lolote litakalotokea.

    Hata hivyo kabla ya kuondoka Kenya alikuwa amefanya utafiti na kupata shule moja ambayo inamfaa mwanawe.

    Kabla ya kujinga na shule hiyo mwananwe aliitaji kutahiniwa ili kuona kama anahitimu na hiyo ilimbidi Beatrice kwamba amfanyie mafunzo nyumbani ili kunoa makali yake.

    Juhudi zake zilifanikiwa.

    Alipofanyiwa mahojiano mwezi Desemba alipita na akijunga na shule.

    Imekuwa ni furaha kwa mama yake.

    "inapendeza sana, kila siku nikimsikia nasema hii ni miujiza ya Mungu hata yeye mwenye ananipatia changamoto na kuniambia tulikuja wakati mmoja na kuanza kusoma wakati mmoja lakini wewe huongei kama mimi. Anaongea kabisa ukimsikiliza kama bado hujamuona utafikiria ni mtoto mchina. Ana marafiki wengi watoto wachina na wanacheza pamoja kila siku. Anaimba nyimbo za kichina na pia kwenye TV anatazama vibozo vya kichina. Saa zingine usiku akilala unamsikia anaota na kichina na nafurahi sana"

    Huyu hapa ni Tephilla.

    Tephila mwenye vazi la machungwaanajumuika na watoto wengine wachina wakati wa sikukuya mwaka mpya wa kichina 2014. Mama yake Betreace anasema anafurahi kwamba mwanawe alijifunza lugha ya kichina ndani ya muda mfupi.

    Beatrice Maisori akiwa na mwanawe Tephilla mwenye umri wa miaka 10. Sasa Tephila anasoma kwenye shule moja mjini Beijing na anaweza kuongea kichina vyema. Anaimba nyimbo za kichina na pia kwenye TV anatazama vibozo (cartoon) vya kichina.

    Beatrice Maisori anasomea biashara ya kimataifa katika chuo kimoja mjini Beijing China. Anafuatilia kwa makini mahusiano ya kibiashara kati ya China na Afrika kupitia kwa majukwaa ya ushirikiano kama vile FOCAC na anaona kuna umuhimu wa kuhamisha teknolojia na hatimaye kuwezesha Kenya kujitegemea katika baadhi ya sekta

    Akiwa sasa ametulia na bila wasiwasi wa masomo ya mtoto wake Beatrice anajitahidi kutimiza lengo lake la kukamilisha shahada ya uzamifu (PhD) katika taaluma ya biashara ya kimataifa.

    Nilimuuliza kwa nini aliamua kuchagua kusomea China.

    "somo langu ni biashara ya kimataifa lakini nyanja ninayofanyia utafiti haswa ni uwekezaji wa China barani Afrika. Ukisomea biashara ya kimataifa unahitaji kufahamu kuhusu kampuni ama mashirika ambayo yanafanya uwekezaji wa moja kwa moja nje ya nchi yao. Kwa miaka kumi ambayo imepita tumeanza kuona uwepo wa wachina barani Afrika unaongezeka. Kumekuwa na kampuni nyingi za serikali lakini sasa pia mashirika ya kibinasfi yameanza kwenda Afrika. Kwa hivyo kwangu ilikuwa ni muhimu kuwa hapa China ndio niweze kusoma hali halisi ya kampuni hizo nikiwa hapa China na kuelewa lugha, utamaduni na mikakati inayowekwa na serikali kuhimiza wawekezaji kwenda Afrika. Pia najifunza zaidi kuhusu uhusiano wa China na Afrika."

    Beatrice anafuatilia kwa makini mahusiano ya kibiashara kati ya China na Afrika kupitia kwa majukwaa ya ushirikiano kama vile FOCAC.

    Ndoto yake ni kuona uwekezaji wa China nchini Kenya ukikua lakini pia anaona kuna umuhimu wa kuhamisha teknolojia na mbinu za ufanyaji biashara na hatimaye kuwezesha Kenya kujitegemea katika baadhi ya sekta.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako