• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Uwekezaji wa nje ni muhimu katika mpango wa "ukanda na barabara"

    (GMT+08:00) 2015-01-21 09:54:40

    Uwekezaji wa China katika nchi za nje unatarajiwa kuwa muhimu katika kusukuma mbele mipango ya barabara na ukanda..Wakati wa kongamano la pili la Uwekezaji wa China katika nchi za nje uliokamilika mwishoni mwa wiki iliyopita, maafisa wa kimataifa na wajasiriamali walisema kuimarisha ushirikiano kati ya wafanyabiashara wa China na wenzao wa nje kunaweza kuongeza nguvu ya mipango ya Rais Xi. Mpango wa mradi wa kufufua barabara ya kale ya Hariri ilipewa kipaumbele na Rais Xi Jinping wakati wa ziara yake nchini Kazakhstan Septemba mwaka 2013, ikiwa ni pamoja na ukanda wa nchi kavu kutoka China kupitia Asia ya Kati na Russia hadi Ulaya, na njia ya bahari kupitia Mlango wa Malacca hadi nchini India, Mashariki ya Kati na Afrika Mashariki.

    Aliyekuwa naibu katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa anayeshughulikia uchumi na jamii Sha Zukang, amesema mpango wa "ukanda na barabara" unahitaji ushirikiano zaidi wa kibiashara, ujenzi wa miundombinu na kubadilishana utamaduni. Amesema mashaka na mgogoro vilijitokeza baada ya mipango hiyo kuanza, lakini muda na mafanikio utathibitisha kwamba, ufahamu wa kila upande na maendeleo pamoja vina thamani ya msingi ya mpango huo mkubwa. China ina mipango ya miradi mikubwa ya kuboresha kuunganishwa.

    Wakati mkutano APEC uliofanyika Beijing mwaka jana, rais Xi Jinping wa China alitangaza kuchangia dola bilioni 40 za kimarekani katika mfuko wa Njia ya Hariri, na kutangaza kwamba hata kabla ya kufufua njia za kale za biashara lazima kuwe na barabara halisi. Amesema hadi pale kutakapokuwa na barabara halisi, usafiri wa watu na bidhaa hautaweza kufanikiwa. Mbali na mfuko huo, Benki ya uwekezaji wa miundombinu ya Asia ambayo inaungwa mkono na China pia itachangia fedha kwa ajili ya ujenzi wa miundombinu. Huku ikiwa na mamlaka ya mtaji wa dola bilioni 100 za kimarekani, Benki hiyo inatarajiwa kuanza kutoa huduma kabla ya mwisho wa mwaka huu. Zhou Jian, ambaye ni mshauri na wizara ya mambo ya nje ya China, alisema wakati wa ufunguzi wa kongamano la APEC kwamba, makampuni ni nguzo katika kukuza mipango ya Rais Xi ya ukanda na barabara. Alipendekeza kufanyika kwa utafiti kabla ya uwekezaji katika nchi zinazolengwa, na kutathmini njia ambazo kila upande utanufaika na pia jukumu na wajibu wa kirafiki wa mawasiliano ya nje.

    Mwenyekiti wa shirika la United World Men Ching alitaka wawekezaji wote wa China kuwa wachangamfu lakini pia kuwa na tahadhari wakati wakifanya biashara katika nchi za nje, ili kutambua njia za kunufaisha kila upande na kuwa na viwango vidogo vya hatari. China sasa iko katika mazungumzo ya mradi wa reli ya kasi ya juu na zaidi ya nchi 28, agenda kuu ikiwa ni kujenga reli ya urefu wa zaidi ya kilomita 5,000.

    Balozi wa Ufaransa Maurice Gourdault-Montagne aliyakaribisha makampuni ya China kuwekeza nchini Ufaransa, hasa katika sekta ya utamaduni na mitindo. Alisema nchi hiyo ina zaidi ya wateja milioni 500, soko la wazi, uwezo wa juu wa kufanya kazi, na wataalam wa ngazi ya juu wa sayansi na teknolojia, mambo yanayotoa mazingira mazuri kwa makampuni ya Kichina.

    Naye balozi wa Pakistan nchini China, Muhammad Salim Khan, alisema mpango wa "ukanda na barabara" unatoa fursa kwa nchi mbili kuanzisha ukanda wa kiuchumi unaozinufaisha pande zote mbili. Alisema ushirikiano baina ya nchi katika kutimiza mipango hiyo utawezesha kupungua kwa umbali wa zaidi ya kilomita 10,000 ikilinganishwa na kutumia njia ya jadi ya biashara kama vile kutoka Urumqi kupitia Khunjerab hadi Dubai. Katika kongamano hilo alisema uwekezaji katika miundombinu ya usafiri wa kikanda inaweza kutoa faida ya hadi dola bilioni 37 za kimarekani ifikapo mwaka wa 2020, na dola bilioni 66 baada ya mwaka huo.

    Wakati huo huo, bwana He Haifeng mkurugenzi wa Kituo cha utafiti wa Sera za Kifedha kwenye taasisi ya Sayansi ya Jamii ya China alisema ukosefu wa uvumbuzi kwenye sekta ya fedha ni kikwazo kwa China katika kupiga hatua kwenye biashara ya kimataifa.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako