• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Mapambano dhidi ya ugaidi yamekuwa changamoto kwa serikali za nchi mbalimbali za Afrika

    (GMT+08:00) 2015-01-27 18:52:53

    Tangu mwanzoni mwa mwaka huu, kundi la kigaidi la Boko Haram la Nigeria limefanya mashambulizi mengi makubwa dhidi ya watu wasio na hatia, ambayo yamefuatiliwa na vyombo vya habari, na kusababisha watu watambue ugumu wa kazi za kupambana na ugaidi inayozikabili serikali za nchi mbalimbali za Afrika.

    Kwa mujibu wa takiwmu zilizotolewa na Umoja wa Afrika, hivi sasa kuna makundi ya kigaidi yasiyopungua 16 barani Afrika, likiwemo kundi la Boko Haram nchini Nigeria na kundi la Al-Shabaab nchini Somalia, na makundi hayo yamefanya mashambulizi mengi ya kigaidi wakati Afrika ikiwa katika msukosuko na mchakato wa mageuzi, na kutumia mbinu na mikakati mpya, na kulenga shabaha mpya. Ili kupambana na ugaidi, Nigeria, Kenya na nchi nyingine zinazoathiriwa zaidi na vitendo vya kigaidi zimechukua hatua kali ili kupambana na makundi hayo, lakini bado kuna matatizo mengi katika operesheni hizi, ikiwa ni pamoja na uwezo mdogo wa kupambana na ugaidi, upungufu wa nguvukazi na zana katika idara za upelelezi, ukosefu wa ushirikiano kati ya serikali za mitaa na idara za polisi. Wachambuzi wanaona kuwa, kama matatizo hayo hayatatatuliwa, hali mbaya ya usalama inayotokana na ugaidi itazidi kuwa mbaya ndani ya muda mfupi.

    Hivi sasa bara la Afrika limekuwa uwanja mpya wa mazoezi kwa magaidi, jumuiya ya kimataifa ina wasiwasi mkubwa na hali ya vita dhidi ya ugaidi. Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa limetoa taarifa likisema, huenda Afrika itakuwa eneo jipya la kuzalisha magaidi ambao wataweza kufanya mashambulizi makubwa ya kigaidi nje ya Afrika. Na Umoja wa Afrika pia ulionya kuwa, mapigano na ugaidi unatishia amani na usalama wa Afrika, na kama havitazuiliwa, maendeleo ya jamii na uchumi yaliyopatikana katika nchi nyingi za Afrika katika miaka ya karibuni yataharibiwa.

    Suala la ugaidi ni changamoto kubwa inayozuia maendeleo ya siasa na uchumi wa Afrika, na makundi ya kigaidi kuibuka na kuendelezwa kunatokana na kukwama kwa maendeleo ya uchumi na pengo kubwa kati ya watu maskini na matajiri. Malalamiko waliyonayo watu kwenye jamii zilizowekwa pembezoni yamesababisha baadhi ya vijana kujiunga na makundi ya kigaidi, na kuhodhi madaraka na ufisadi zimekuwa ni sababu za kisiasa za kuibuka kwa ugaidi.

    Makundi ya kigaidi ya Boko Haram na Al-Shabaab sio tu yanatishia usalama wa Afrika, bali pia maslahi ya nchi za nje barani Afrika. Wachambuzi wanaona kuwa, hivi sasa ili kupambana na ugaidi, ni lazima kufanya juhudi ili kutatua hali ya kutokuwa na zana za kisasa za kijeshi na ukosefu wa taarifa za ujasusi, na kutumia vizuri nguvu za nchi, kanda na jumuiya ya kimataifa, na wakati kiwango cha maendeleo ya jamii na uchumi na uwezo wa serikali wa usimamizi na udhibiti wa migogoro unapoongezeka, ndipo vita dhidi ya ugaidi vitakapofanikiwa.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako