• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Chai ya yasmini--zao muhimu la biashara ya nje la mji wa Fuzhou

    (GMT+08:00) 2015-01-28 10:17:25

    Ukionja chai ya yasmini iliyozalishwa mjini Fuzhou, harufu nzuri kwenye kinywa chako itakufanya kujihisi kama uko katika mbuga yenye maua mengi.

    Katika enzi ya Han (mwaka 202KK-9BK), chai ya yasmini iliingizwa nchini China kutoka Rome kupitia njia ya hariri ya baharini, mimea ya yasmini haikui katika eneo baridi, hivyo mji wa Fuzhou wenye hali ya hewa ya fufutende ulikuwa moja kati ya maeneo yaliyoshughulikia kilimo cha yasmini mapema zaidi nchini China.

    Meneja mkuu wa kampuni ya Chunlun ya Fujian Bw. Fu Tianlong anasema, mji wa Fuzhou ulivumbua njia pekee ya kuzalisha chai ya yasmini katika enzi ya Song (mwaka 960 -1279), ladha ya chai na maua ya yasmini vilichanganywa vizuri na chai hiyo ilikuwa maarufu sana.

    Uzalishaji wa chai ya yasmini unahitaji hatua zaidi ya kumi na unachukua muda mrefu. Naibu mkuu wa kiwanda cha chai cha Fuzhou Bw. Lin Nairong anasema, hatua hizi ni pamoja na kusindikiza chai, kuvuna maua, kuchanganya chai na maua, kukoroga mchanganyiko, na kukausha chai. Kama hatua yoyote ikikosewa, itaathiri manukato na ladhaa ya chai.

    Wakati China inapokuwa katika majira ya baridi, hali ya hewa ya mji wa Fuzhou bado ni zaidi ya nyuzi 15. Meneja mkuu wa kampuni ya Minrong Bw. Wang Dexing anasema, kando ya mto Mingjiang ni tambarare na ardhi oevu, na kuna rutuba nyingi. Eneo hili pia lina mwanga wa kutosha wa jua na mazingira mazuri, hivyo maua ya yasmini yanayozalishwa huko yananukia sana. Hivi sasa kuna mashamba ya yasmini yenye ukubwa wa hekta 1200 mjini Fuzhou, ambayo mengi yako katika ardhi oevu kando ya mto Mingjiang na mto Wulongjiang.

    Majira ya joto ni wakati mzuri zaidi wa kuvuna yasmini, wafanyakazi wanapilikapilika za kuzalisha chai ya yasmini. Bw. Lin Nairong anasema wafanyakazi wanachanganya chai na maua ili kuifanya iwe na harufu ya yasmini na yasmini iwe na ladha ya chai. Wafanyakazi si kama tu wanatakiwa kuamua ukubwa wa malundiko ya chai, bali pia wanatakiwa kutilia maanani kiwango cha joto la chai. Bw. Wang Dexing anasema mabadiliko ya hali ya hewa na mwanga wa jua yanayafanya maua yachanue katika siku tofauti na kipekee. Hivyo wafanyakazi wanahitaji uzoefu mkubwa kuamua wakati wa kuvuna maua.

    Kwa kawaida chai ya yasmini ya Fuzhou inasindikizwa mara tatu, lakini chai ya ngazi ya juu zaidi inatakiwa kusindikizwa mara saba had nane, na kuifanya iwe na harufu ya yasmini bila maua yenyewe kuonekana. Mazingira mazuri ya kipekee na ufundi wa jadi umeifanya chai ya yasmini iwe na sifa ya kipekee. Mkuu wa shirika la mawasiliano ya chai ya mlango wa bahari wa Fuzhou Bw. Wu Yidian anasema chai ya yasmini imekuwa zao muhimu linalouzwa nje tokea enzi ya Song. Biashara hiyo ilifikia kilele chake katika enzi ya Qing (mwaka 1636 - 1912) hasa baada ya mji wa Fuzhou kuwa bandari ya biashara huria.

    Mkurugenzi wa ofisi ya idara ya kilimo ya mji wa Fuzhou Bw. Zheng Jiangmin anasema, katika miaka ya hivi karibuni, mji wa Fuzhou umeunga mkono maendeleo ya kilimo cha chai ya yasmini, na kujitahidi kuifanya bidhaa hiyo iwe alama ya mji huo. Mji huo umetunga sheria na kanuni kuhusu urithi wa ufundi wa kuzalisha chai ya yasmini, na uhifadhi wa mashamba ya yasmini na matangazo ya bidhaa hiyo. Serikali pia imetoa ruzuku kwa wakulima wanaoshughulikia kilimo cha yasmini, kuyaunga mkono makampuni ya chai kuanzisha chapa maarufu, na kusukuma mbele utafiti kuhusu chai ya yasmini.

    Hivi sasa chai ya yasmini imekuwa alama maarufu ya mji wa Fuzhou. Mwaka 2011, shirika la chai la kimataifa liliupa mji wa Fuzhou sifa ya "chanzo cha chai ya yasmini duniani". Mwaka 2014, wizara ya utamaduni ya China iliiweka chai ya yasmini ya Fuzhou kwenye orodha ya uhifadhi wa urithi wa kiutamaduni usioonekana ya China, pia imewekwa na Shirika la Chakula na Kilimo la Umoja wa Mataifa kwenye orodha ya uridhi muhimu wa utamaduni wa kilimo duniani.

    Wakati China inapoongeza nguvu kujenga "Ukanda wa kiuchumi wa njia ya hariri baharini" na "Njia ya hariri baharini ya karne ya 21", chai ya yasmini ya mji wa Fuzhou yenye historia ya miaka elfu 1 itaingia tena kwenye soko la kimataifa. Meneja mkuu wa kampuni ya chai ya Mantangxiang ya Fuzhou Bw. Gao Chengsheng alisema, kampuni yake itawapatia wateja chai ya yasmini ambayo inanukia na kutokuwa na uchafuzi, kuwaonesha wageni ufundi wa kuzalisha chai hiyo, na kutangaza utamaduni wa China wenye mvuto wa kipekee.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako