• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Uwepo wa ndege wa majini ni ishara ya mazingira ya ardhi oevu

    (GMT+08:00) 2015-01-28 10:17:52

    Bw. Yi Feiyue mwenye umri wa miaka 45 ni mkuu wa kituo cha usimamizi wa ziwa Caisang katika hifadhi ya kitaifa ya ziwa Dongting Mashariki mkoani Hunan. Anapenda kuangalia ndege wa majini kwa darubini.

    Ziwa Dongting liko katika maeneo ya katikati na chini ya mto Changjiang, na ni moja kati ya maskani ya ndege wa majini, ambapo kila ifikapo mwezi Septemba, ndege zaidi ya laki moja wanafika ziwa hili kutoka kaskazini.

    Lakini hivi karibuni Bw. Yi Feiyue aligundua kuwa idadi ya bata maji wenye alama nyeupe kwenye paji la uso (Anser albifrons) imepungua. Miaka mitano iliyopita, ndege hao kutoka Siberia walikuwa wakionekana kila siku, lakini katika miaka ya hivi karibuni wanaonekana mara moja kwa wiki. Ana wasiwasi kuwa mazingira ya ardhi oevu huenda yana matatizo.

    Wanasayansi wanafuatilia kujua chanzo cha kupungua kwa kiasi kikubwa kwa bata maji hao. Mtafiti wa kituo cha utafiti wa mazingira cha taasisi ya sayansi ya China Bibi. Cao Lei alisema, kutokana na ujenzi wa mabomba ya maji, kina cha maji katika ziwa Dongting kilipungua mapema zaidi katika majira ya mpukutiko, na kuifanya mafunjo yakue mapema zaidi kwenye ardhi oevu kando ya ziwa hili. Mafunjo hayo yanayopevuka hayakidhi mahitaji ya bata maji hao ambao wanakula machipuko ya mafunjo tu. Hii ni sababu muhimu ya kupungua kwa ndege hawa wanaoishi katika ziwa Dongting wakati wa majira ya baridi. Bibi Cao Lei amesema, aina na idadi ya ndege wa majini ni ishara ya mazingira ya ardhi oevu, Na kupungua kwa bata maji hao kumeonesha kuwa mazingira ya ziwa Dongting yamekuwa makavu zaidi.

    Mpango mkakati wa China wa kuhifadhi aina mbalimbali za viumbe uliotolewa mwaka 2010 unaonesha kuwa, mazingira ya mbuga, maziwa na ardhi oevu yanakuwa mabaya siku hadi siku. Ili kuhifadhi ndege wa majini na mazingira ya ardhi oevu, mwezi Januari mwaka huu idara ya misitu ya China na mfuko wa wanayampori duniani WWF vilianza uchunguzi wa mara ya nne wa ndege wa majini katika maeneo ya katikati na chini ya mto Changjiang, na maziwa kadhaa yakiwemo ziwa Dongting, Ziwa Honghu na Ziwa Boyang yatachunguzwa. Uchunguzi uliopita ulifanyika mwaka 2004, mwaka 2005 na mwaka 2011.

    Bw. Yi Feiyue ameshiriki kwenye uchunguzi huu, na baada ya kufanya uchunguzi kwa siku tatu, aliangalia ardhi oevu zenye ukubwa wa hekta elfu 20, na kugundua ndege 37,719. Bw. Yi Feiyue anafurahia kazi hii inayoonekana ni ya kuchosha. Hivi karibuni aligundua ndege mmoja wa aina ya Dalmatian kwa darubini, ambao hajaonekana kwenye eneo hilo kwa karibu miaka kumi.

    Katika miongo kadhaa iliyopita, Wachina waliendeleza uchumi bila ya kuhifadhi mazingira, na kutokana na athari za kuharibika kwa mazingira zinazotokea sasa, wachina wameanza kuangalia upya vitendo vyao, na kuwa na wazo la kuhifadhi mazingira.

    Mkurugenzi wa hifadhi ya kitaifa ya ziwa Dongting lililoko Mashariki mwa mkoa wa Hunan Bw. Zhao Qihong alisema, zamani watu wengi waliweka nyavu za kuvulia samaki sehemu mbalimbali kwenye ziwa Dongting, na kuwalisha sumu ndege pori. Sasa uwindaji, uvuvi, na uchimbaji wa mchanga vimepigwa marufuku katika eneo muhimu la hifadhi hiyo, na katika maeneo mengine, watu wanaishi kwa masikilizano katika mazingira ya kimaumbile.

    Baadhi ya watu wamekuwa mashabiki ya kuangalia ndege. Bw. Lei Jinyu ni mmoja kati yao. Ametembea karibu maskani yote ya ndege nchini China. Alisema ameangalia aina 962 kati ya aina 1435 za ndege nchini China, na kila anapoangalia aina mpya ya ndege, anarekodi kwenye orodha yake. Sasa hamu yake ya kuangalia ndege imemfanya apate kazi inayohusu ndege, kwani amekuwa meneja wa mradi wa mfuko wa wanyamapori duniani wa kuhifadhi ndege wa majini na ardhi oevu katika eneo la mto Changjiang.

    Bw. Jiang Yong alisema ushabiki wa kuangalia ndege ni nguvu muhimu ya kuhifadhi ardhi oevu na wanayamapori kwenye jamii, na kama China inataka kuhifadhi mazingira vizuri zaidi, inatakiwa kutunga sheria husika.

    Kwenye mkutano wa kamati ya kitaifa ya kuhifadhi aina mbalimbali za viumbe uliofanyika mwezi Desemba mwaka jana, naibu waziri mkuu wa China Bw. Zhang Gaoli alisisitiza kuwa China itatekeleza mradi wa kuhifadhi aina mbalimbali za viumbe katika pande zote, na kuharakisha utungaji wa sheria kuhusu hifadhi za mazingira ya kimaubile.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako