• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Miji mingi iliyoko kwenye Njia ya Hariri yatazamiwa kustawi

    (GMT+08:00) 2015-01-28 19:08:07

    Ripoti iliyotolewa na Taasisi ya Sayansi ya Jamii ya Shanghai, nchini China inatabiri kuwa miji mingi iliyoko kwenye Njia Kongwe ya Hariri na Njia Mpya ya Hariri itastawi kufuatia utekelezaji wa mkakati wa "Ukanda Mmoja Njia Moja" unaohimizwa na China.

    Ripoti hiyo inasema, mwaka 2014 China ilitoa dola za kimarekani bilioni 40 kuanzisha mfuko wa Njia ya Hariri, ambao ni moja ya mpango wa kifedha unaoshirikisha Benki ya Uwekezaji wa Miundo Mbinu ya Asia, Benki ya Maendeleo ya nchi za BRICS, na Benki ya Maendelo ya Jumuiya ya Ushirikiano wa Shanghai. Ripoti hiyo pia imesema, mpango wa kimkakati kuhusu Ukanda wa Kiuchumi wa Njia ya Hariri na Njia ya Hariri Baharini umeingia katika kipindi cha utelekezaji kihalisi.

    Wakati huohuo, takwimu zilizotolewa na Idara Kuu ya Forodha ya China zinaonesha kuwa, mwaka huu idara hiyo itatunga na kutekeleza mpango wa utekelezaji wa mkakati wa "Ukanda Mmoja na Njia Moja", na kuzidisha ushirikiano na forodha za nchi zilizopo kwenye ukanda na njia hiyo.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako