• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • China kuendeleza biashara ya nje ya reli na nguvu ya nyuklia

    (GMT+08:00) 2015-01-28 21:02:11

    Baraza la serikali la China limetangaza mpango wa kuendeleza biashara ya nje ya reli ya mwendo kasi, nguvu ya nyuklia, na vifaa vya ujenzi.

    Katika taarifa iliyotolewa kwenye tovuti ya serikali, baraza hilo limesema idara za serikali na makampuni zinapaswa kuisaidia China kuingia kwenye soko la kimataifa kwa kuongeza biashara ya nje, ushirikiano katika uwekezaji, na kusukuma mbele mageuzi ya uchumi wa ndani.

    Mwaka jana, uwekezaji wa China katika nchi za nje ulifikia dola za kimarekani bilioni 102.89, ikiwa ni ongezeko la asilimia 14.1 ikilinganishwa na mwaka 2013.

    Taarifa hiyo imesema, China itaunga mkono sekta ya viwanda vya chuma, nguo, na vifaa vya ujenzi kuanzisha utaratibu wa usafirishaji wa bidhaa za China pamoja na teknolojia na vigezo.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako