• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Nigeria yathibitisha mlipuko wa homa ya mafua ya ndege katika majimbo 11

    (GMT+08:00) 2015-01-29 10:25:09

    Serikali ya Nigeria jana ilithibitisha kutokea kwa mlipuko wa homa ya mafua ya ndege katika majimbo 11.

    Hayo yamethibitishwa na waziri wa kilimo na maendeleo ya mji Akinwumi Adesina katika mkutano wa dharura na makamishna wa kilimo wa Abuja huko Nigeria. Ametangaza kwamba serikali imeidhinisha pesa za kuwafidia wakulima wote walioathiriwa na ugonjwa huo.

    Miongoni mwa majimbo yaliyoathiriwa zaidi na mlipuko huo ni pamoja na Lagos, Delta na Plateau. Kwa mujibu wa waziri huyo hadi Januari 27, jumla ya ndege laki 2.3 wameambukizwa, na elfu 51.4 wamekufa.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako