• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Marais wa Sudan na Chad waeleza wasiwasi kuhusu hali ya usalama ya kanda hiyo

    (GMT+08:00) 2015-01-29 10:34:10

    Rais Omer al bashir wa Sudan amefanya mazungumzo na mwenzake wa Chad Bw. Idriss Deby aliyeko ziarani nchini Sudan katika mji wa Khartoum, wakieleza wasiwasi kuhusu hali ya Libya, Sudan Kusini, Jamhuri ya Afrika Kati na Nigeria, na kusema mazungumzo ni njia bora kabisa kutatua mgogoro wa Darfur.

    Bw. Bashir amesema yeye na mgeni wake wamejadilina kuhusu masuala ya kikanda, haswa ya usalama yanayoziathiri kwa pamoja Sudan na Chad.

    Kwa upande wake Bw. Deby amesisitiza kuwa Chad inapenda kuona mgogoro wa Darfur unatatuliwa kwa hatua mwafaka, na kusema mazungumzo ni njia nzuri ya kutatua mgogoro na kumaliza maumivu ya watu wa kanda hiyo.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako