• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Kuwawezesha wanawake, Ebola na usalama ni ajenda kuu za mkutano wa Umoja wa Afrika

    (GMT+08:00) 2015-01-29 10:39:37

    Kamati ya Umoja wa Afrika imesema kwenye mkutano mkuu wa Umoja huo unaofanyika mjini Addis Ababa, Ethiopia viongozi wanatarajia kujadili changamoto zilizopo katika kuwawezesha wanawake, mlipuko wa ugonjwa wa Ebola na changamoto za usalama zinazolikabili bara hilo.

    Makamu mwenyekiti wa kamati ya Umoja wa Afrika Bw Erastus Mwencha amesema mwaka jana ulikuwa na changamoto nyingi ikiwa ni pamoja na mlipuko wa ugonjwa wa Ebola, kupungua kwa bei ya bidhaa na changamoto zilizoletwa na kundi la Boko Haram.

    Mbali na hayo, mkutano huo pia utazindua ruwaza ya 2063 yenye lengo la kuweka mipango ya kufanya mageuzi ya uchumi wa Afrika kwa miaka 50 ijayo, pamoja na mipango ya miaka 10. Mwaka huu utekelezaji wa mipango ya maendeleo ya Milenia utafika mwisho, Bw Mwencha amesema ruwaza ya 2063 inahusu mambo baada ya kwisha kwa utekelezaji wa malengo ya milenia.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako