• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Bahati nasibu itaamua hatma ya Guinea na Mali, Ivory Coast yaingia robo fainali

    (GMT+08:00) 2015-01-29 13:57:54
    Matokeo ya bahati nasibu yataamuwa kama ni Guinea au Mali itakayotinga robo fainali katika michuano ya kombe la mataifa ya Afrika baada ya timu hizo kutoka sare ya 1-1 huko Magomo nchini Guinea ya Ikweta. Bahati nasibu hiyo imeahirishwa hadi leo Alhamis, ambapo awali ilitakiwa kufanyika jana jioni. Katika bahati nasibu CAF itaweka majina ya timu mbili ndani ya mipira miwili kabla ya ofisa kualikwa kuchagua mpira, ambapo kutakuwa na jina la timu itakayoingia robo fainali, na itakabiliana na Ghana Jumapili mchana. Wakati huohuo Ivory Coast imemaliza mechi za kundi D wakiwa vinara baada ya kuichapa Cameroon kwa goli 1-0, mechi pekee kwenye kundi hilo iliyoisha bila ya kupata sare ya 1-1. Kama timu hizo zingetoka sare nazo pia zingeingia kwenye bahati nasibu.
    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako