• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • China kuongeza usimamizi kwa bidhaa feki zinazouzwa kupitia mtandao wa internet

    (GMT+08:00) 2015-01-29 17:09:22

    Wizara ya Biashara ya China imeitisha mkutano na waandishi wa habari ili kujibu masuala yaliyogonga vichwa vya habari hivi karibuni. Kuhusu suala la uuzaji wa bidhaa feki kupitia mtandao wa internet, msemaji wa wizara hiyo Bw. Shen Danyang amesema China itatumia teknolojia mpya kuongeza usimamizi dhidi ya suala hilo.

    Bw. Shen amesema masuala kama uuzaji wa bidhaa feki na vitendo vya kukiuka hakimiliki katika mtandao wa internet yanaibuka na kutoa athari mbaya kufuatia maendeleo ya kasi ya biashara ya kielektroniki ya China na utatuzi wa suala hilo unahitaji juhudi za pamoja za serikali, makampuni, wateja na sekta mbalimbali za jamii.

    Anasema, (sauti 1) "Wizara ya biashara itaongeza usimamizi kwa vitendo vya kuuza bidhaa feki na kukiuka hakimiliki kupitia mtandao wa internet kwa kupitia kukamilisha sheria na taratibu kuhusu biashara ya kielektroniki, kutumia teknolojia mpya kuongeza uwezo wa kusimamia soko, kuzidisha ushirikiano kati ya serikali na makampuni na kuongeza uwezo wa kuzuia vitendo vya kukiuka hakimiliki na uuzaji wa bidhaa feki, na kuwafanya wateja wawe na mwamko na uwezo wa kutambua bidhaa feki."

    Mbali na uuzaji wa bidhaa feki na vitendo vya kukiuka hakimiliki kwenye mtandao wa internet, Bw. Shen pia amezungumzia migogoro ya kibiashara kati ya China na Marekani kuhusu suala la matairi. Habari zinasema Wizara ya Biashara ya Marekani tarehe 21 iliamua kutoza ushuru mkubwa matairi yanazouzwa na makampuni ya China nchini Marekani kwa madai kuwa bidhaa hizo zinauzwa kwa wingi na bei ya chini mno. Akizungumzia suala hilo, Bw. Shen anasema uamuzi wa Marekani hauna usawa na haki. (sauti 2)

    "Mwaka 2009, Marekani imewahi kufanya hivyo dhidi ya matairi ya China na kuuletea hasara kubwa uhusiano wa kiuchumi na kibiashara kati ya nchi hizo mbili, na China inaitaka Marekani ijifunze uzoefu huo kushughulikia kwa uangalifu kesi hiyo, ili kuepusha uharibifu tena wa biashara na ushirikiano kati ya nchi mbili."

    Kuhusu Benki Kuu ya Umoja wa Ulaya hivi karibuni kutangaza sera ya kuongeza fedha kwenye mzunguko, Bw. Shen anasema hatua hiyo hakika itakuwa na athari ya moja ya moja kwa biashara kati ya China na umoja huo.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako