• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Nchi za Asia ya Kati zanufaika na mpango wa China kuhusu ujenzi wa eneo la uchumi la Njia ya Hariri

    (GMT+08:00) 2015-02-04 15:30:57

    Nchi za Asia ya Kati zimefuatiliwa sana na vyombo vya habari duniani Baada ya viongozi wa China kutoa mpango wa kimkakati kuhusu kuanzisha eneo la uchumi la Njia ya Hariri na Njia ya Hariri baharini katika karne ya 21. Kuanzisha eneo la uchumi la Njia ya Hariri, bila shaka kutatoa fursa kubwa zaidi ya maendeleo ya eneo la Asia ya Kati lililoko kati ya bara la Asia na Ulaya.

    Ikiwa sehemu moja muhimu ya historia ya mawasiliano ya binadamu, Njia ya Hariri ya asili inafuatiliwa sana. Kwa mfano, Japan ilitoa mkakati mpya wa diplomasia ya Njia ya Hariri miaka 90 ya karne iliyopita, na Marekani ilitoa mpango wa Njia mpya ya Hariri miaka 4 iliyopita. Lakini mipango hiyo ilitolewa kutokana na maslahi ya nchi hizo kubwa, na haijafuatilia maendeleo ya muda mrefu ya eneo la Asia ya Kati.

    Hivi sasa dunia inaendelea kufungamana, na ushirikiano wa uchumi wa kikanda unaendelea kwa kasi, nchi mbalimbali za Asia ya Kati zinazochukuliwa kuwa ni sehemu muhimu ya kimkakati zinakabiliwa na majukumu ya kurekebisha miundo ya uchumi na kuongeza nguvu ya taifa.

    Rais Xi Jinping wa China alipofanya ziara nchini Mongolia mwezi Agosti mwaka jana, alisema China inapenda kutoa fursa ya maendeleo kwa nchi jirani ikiwemo Mongolia. Aliongeza kuwa China inakaribisha nchi jirani kujiendeleza kwa kutumia fursa ya maendeleo ya China.

    Mpango kuhusu eneo la uchumi la Njia ya Hariri na Njia ya Hariri baharini, umetolewa na rais wa China kwa msingi wa kuleta maendeleo ya uchumi, ukilenga kufanya ushirikiano wa kiuchumi. Mpango huo unalingana na mahitaji ya haraka ya nchi zilizoko kwenye Njia ya Hariri ya asili kuhusu kupata maendeleo ya pamoja, na umeleta fursa mpya kwa China na nchi hizo kushirikiana na kunufaika kwa pamoja. Huu ni wakati mwafaka kwa nchi za Asia ya Kati kutumia fursa ya mpango huo wa China.

    Nchi tano za Asia ya Kati yaani Kazakhstan,Uzbekistan,Kyrgyzstan, Tajikistan, na Turkmenistan ambazo zina eneo la kilomita milioni 4 za mraba ziko kwenye sehemu muhimu kati ya bara la Asia na Ulaya, na zilikuwa kituo muhimu cha Njia ya Hariri ya asili. Nchi hizo zina maliasili nyingi za mafuta, gesi, madini na raslimali ya utalii, lakini ni nchi zisizopakana na bahari, mawasiliano ya barabara yako nyuma, na zina kiwango cha chini cha maendeleo ya uchumi kuliko nchi za Asia Mashariki na Ulaya.

    China ni jirani wa nchi hizo. Njia ya Hariri ya asili, ferghana horse wa Turkmenistan, mabomba ya kusafirisha mafuta na gesi kutoka Kazakhstan hadi China, na mtaa wa Deng Xiaoping nchini Kyrgyzstan, zimeshuhudia mawasiliano ya karibu kati ya China na nchi hizo za Asia ya Kati katika miaka zaidi ya 2,000 iliyopita, ambayo ni msingi wa kiutamaduni na kijamii wa kujenga eneo la uchumi la Njia ya Hariri.

    Kwa nchi za Asia ya Kati, mpango wa eneo la uchumi la Njia ya Hariri na Njia ya Hariri baharini utazisaidia kuboresha mawasiliano ya barabara. Eneo la Asia ya Kati halipakani na bahari, hali hii ni kikwazo cha maendeleo ya uchumi wa nchi za Asia ya Kati. Lakini mpango wa eneo la uchumi la Njia ya Hariri si kama tu utaifanya Asia ya Kati iwe njia yenye urahisi inayounganisha kanda ya Asia na Pasifiki na bara la Ulaya, bali pia utaleta uwezekano kwa nchi za Asia ya Kati katika kupanua mawasiliano kati yao na nchi nyingine na kuimarisha ushirikiano wa kimataifa.

    Konsela wa biashara wa ubalozi wa Tajikistan nchini China hivi karibuni alipohudhuria mkutano wa pili wa uwekezaji wa China kwa nchi za nje alisema, ikiwa ni nchi yenye nguvu kubwa kiuchumi, China imetoa mpango wa kustawisha upya Njia ya Hariri, na hii ni hatua muhimu kwa ushirikiano na mawasiliano kati ya nchi mbalimbali za Asia ya Kati. Aliongeza kuwa kama mpango huo utatekelezwa, utakuwa na faida kubwa kwa nchi mbalimbali za Asia ya Kati ikiwemo Tajikistan, hivyo nchi za Asia ya Kati zinatilia maanani sana mwito uliotolewa na China.

    Lakini je, mpango wa eneo la uchumi la Njia ya Hariri na Njia ya Hariri baharini utaleta fursa zipi kwa eneo la Asia ya Kati?

    Kwa upande wa ushirikiano wa kiuchumi, China na nchi za Asia ya Kati zina maslahi ya pamoja. Pande mbili hizo zinasaidiana kwenye maliasili, miundo ya uchumi, na bidhaa za viwanda na mazao ya kilimo, ustawi wa biashara za bidhaa na huduma utazisaidia pande hizo kuongeza thamani ya biashara kati yao, utahimiza maendeleo ya sekta za utengenezaji bidhaa na huduma za nchi mbalimbali, na hivyo kuongeza nafasi za ajira.

    Wakati huo huo, nchi za Asia ya Kati zina maliasili nyingi ya mafuta, gesi na madini, pia zina raslimali ya nguvu kazi yenye gharama ndogo, na China ni soko zuri kwao. Aidha ardhi zinaozopakana zinatoa urahisi kwa usafirishaji wa bidhaa.

    Takwimu zinaonesha kuwa China imekuwa mwenzi mkubwa zaidi wa biashara wa Kazakhstan na Turkmenistan, ni mwenzi mkubwa wa pili wa biashara wa Uzbekistan na Kyrgyzstan. Mawasiliano ya karibu ya kiuchumi kati ya China na Asia ya Kati ni msingi halisi kwa nchi za Asia ya Kati kushiriki kwenye utekelezaji wa mpango wa ujenzi wa eneo la uchumi la Njia Hariri.

    China ni nchi ya pili yenye nguvu kubwa ya uchumi duniani, ni soko kubwa la pili duniani na ina akiba kubwa zaidi ya fedha za kigeni, pia ina sekta nyingi zilizopiga hatua kiteknolojia, vilevile ina uzoefu mkubwa katika ujenzi wa miundo mbinu. China pia ina uwezo wa kutosha kutoa fursa ya maendeleo kwa nchi zilizo kwenye Njia ya Hariri zikiwemo nchi tano za Asia ya Kati. Takwimu husika zinaonesha kuwa, mwaka 2013 thamani ya biashara kati ya China na nchi zilizo kwenye eneo la uchumi wa Njia ya Hariri na Njia ya Hariri baharini ilikuwa ni zaidi ya dola za kimarekani trilioni 1 ambayo ni asilimia 25 ya thamani ya jumla ya biashara kati ya China na nchi za nje.

    Katika miaka ya hivi karibuni, mafanikio mengi yamepatikana katika juhudi za kuboresha mawasiliano kati ya China na nchi za Asia ya Kati. Kwa mfano, reli mbili zimejengwa kuunganisha Asia na Ulaya zikipita sehemu ya Asia ya Kati, China imeanzisha safari za ndege ya moja kwa moja kati yake na Kazakhstan,Uzbekistan na Tajikistan, na mradi wa kipindi cha kwanza wa kituo cha ushirikiano cha usafirishaji wa mizigo kati ya China na Kazakhstan ulizinduliwa mwezi Mei mwaka jana.

    Hatua zinazochukuliwa na China ikiwemo kutoa mwito wa kuanzisha mfuko wa Njia ya Hariri na Benki ya Uwekezaji wa Miundo mbinu ya Asia, zitazifanya nchi tano za Asia ya Kati na nchi nyingine jirani zinufaike na mageuzi na maendeleo ya China, na kuuwezesha mpango wa kimkakati wa ujenzi wa eneo la uchumi la Njia ya Hariri na Njia ya Hariri baharini utekelezwe hatua kwa hatua.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako