• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • OECD yasema mageuzi nchini China yapata maendeleo dhahiri

    (GMT+08:00) 2015-02-10 18:33:45

    Jumuia ya Ushirikiano wa Uchumi na Maendeleo OECD imesema, mageuzi nchini China katika miaka ya karibuni kwenye sekta muhimu yamepata maendeleo dhahiri. Kwa mujibu wa ripoti iliyotolewa jana na Jumuiya hiyo kuhusu tathmini ya mageuzi ya muundo wa kiuchumi katika nchi mbalimbali mwaka 2015, kuanzia mwaka 2008 hadi mwaka 2013, pengo kati ya pato la taifa la China kwa mtu mmoja mmoja na lile katika nchi wanachama wa OECD zinazoendelea zaidi kiuchumi linapungua. Sekta nyingi zimeanza kuwa wazi kwa wawekezaji binafsi, utaratibu wa kuidhinisha mitaji ya kigeni umekuwa rahisi zaidi, elimu ya kiwango cha juu inazingatia zaidi ubora badala ya kupanuka kwa ukubwa wake, na vilevile mageuzi ya kiwango cha riba yamewafanya wateja wapate fedha nyingi zaidi.

    OECD pia imesema, miji mingi zaidi nchini China imeanza kutoa huduma bora za jamii siku hadi siku kwa vibarua wanaohama hama katika miji mbalimbali nchini, hatua hiyo sio tu inasaidia kuongeza nguvu ya manunuzi ya wafanyakazi hao, bali pia inasaidia uchumi wa China kuongezeka kwa uwiano.

    Hata hivyom OECD imesema mageuzi yanatakiwa kuimarishwa zaidi nchini China, ambayo ni pamoja na kuweka mazingira mazuri kwa kampuni ili ziweze kujiendeleza kwa usawa, kupunguza idara za mambo ya utawala kuingilia mambo ya kiuchumi, kulinganisha elimu ya kiwango cha juu na mahitaji ya soko la nguvukazi, na kudhibiti vitendo vya kujipatia faida wakati wa kusimamia mageuzi ya kifedha.

    Takwimu zilizotolewa na OECD zinaonesha kuwa, mbali na China, uchumi wa makundi mengine makubwa ya kiuchumi zikiwemo Marekani, Japan na Brazil unaelekea kuongezeka kwa utulivu, na ukuaji wa uchumi katika eneo linalotumia Euro unaonesha ishara nzuri.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako