• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Waziri mkuu wa China afanya mazungumzo na wataalamu wa kigeni

    (GMT+08:00) 2015-02-11 10:49:48

    Waziri mkuu wa China Bw. Li Keqiang jana alasiri alifanya mazungumzo na wataalamu wa kigeni na kusikiliza maoni na mapendekezo yao kuhusu maendeleo ya kiuchumi na kijamii ya China.

    Kwenye mkutano huo Bw. Li Keqiang alisema, maendeleo ya China yanahitaji maoni na busara za pande zote, kwa hiyo China itaongeza nguvu zaidi katika kuingiza wataalamu kutoka nje, na kuwafanya wapende kuja na kuishi nchini China. Bw. Li amewashukuru wataalamu wa kigeni kwa michango yao kwa ajili ya maendeleo ya China, na kusema China itapunguza ugumu wa kuingiza wataalamu kutoka nchi za nje.

    "Kuna msemo wa kale wa kichina unaosema ukubwa wa bahari unatokana na kuwa inakusanya maji kutoka mito na mifereji yote. Maendeleo ya China yanahitaji watalaam wa nyanja mbalimbali, na pia yanahitaji kukusanya maoni na busara za pande zote. Tutaendelea kuongeza nguvu ya kuingiza wataalamu kutoka nje, kuwavutia wataalamu wengi kuja China na kuwarahisishia kazi na maisha yao nchini China."

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako