• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Siku ya kwanza ya mwaka mpya wa jadi wa China

    Sikukuu ya Spring ni mwaka mpya kwa kalenda ya jadi ya China, ambayo ni sikukuu kubwa kabisa katika jamii ya Wachina walioko kila pembe ya dunia. Sikukuu ya Spring ni ishara ya kumalizika kwa muda mrefu wa siku za baridi kali na kuwadia kwa majira ya Spring, ambapo uhai na ustawi hurudi katika sehemu ya kaskazini ya dunia hii. Baada ya kuishi na baridi kali kwa zaidi ya miezi mitatu, binadamu wanaokaa sehemu ya kaskazini mwa dunia wanatamani sana majira ya Spring yafike, majira ambayo baridi huanza kupungua, mimea ya kila aina inachipuka na maua yanachanua.

     

    Mwaka 2015: Mwaka wa Mbuzi

    Kwa mujibu wa kalenda ya kilimo ya China, leo ni siku ya pili ya mwaka mpya wa 2015, ambao pia ni mwaka wa Mbuzi. Katika kipindi hiki, tutazungumzia kuhusu mzunguko wa miaka na chanzo cha mwaka wa mbuzi katika kalenda hiyo ya jadi ya China. Katika utamaduni wa Kichina, kundi la wanyama 12 linatumika katika kuhesabu mwaka. Kila mnyama anawakilisha mwaka mmoja, na kila baada ya miaka 12 mzunguko huo unarudia. Utaratibu wa Wanyama hao 12 ni panya, ng'ombe, chui, sungura, dragoni, nyoka, farasi, mbuzi, kima, kuku, mbwa, na nguruwe.

     

    Namna ya kusalimiana wakati wa mwaka mpya wa jadi wa China

    Kutakiana heri ya mwaka mpya ni desturi muhimu katika jamii ya wachina. Watoto wadogo wanawatakia heri na baraka wakubwa, jamaa na marafiki wanatembeleana na kusalimiana, na kusherehekea sikukuu hiyo kupitia kuambiana maneno hayo yenye baraka. Hadithi inasema kuwa zamani watu waliogopa mnyama wa ajabu aiitwaye "nian" aliyekula binadamu kila ilipofika usiku wa mkesha wa mwaka mpya, hivyo walificha nyumbani usiku kucha na kutoka nje baada ya jua kuchomoza ambapo mnyama huyo alikuwa ameondoka, watu wakasalimiana na kutakiana heri kwani walikuwa bado uhai. Inasemekana kuwa huu ndio mwanzo wa desturi ya kutakiana heri katika siku ya kwanza ya mwaka mpya.

     

    Mtindo mpya wa kusherehekea mwaka mpya wa jadi wa China

    Siku ya mwaka mpya wa jadi wa China ni sikukuu ya jadi inayothaminiwa sana na wachina. Katika miaka zaidi ya elfu moja iliyopita, wachina walikuwa na mila na desturi mbalimbali za kusherehekea sikukuu hiyo, lakini kutokana na maendeleo ya jamii na uchumi, mila na desturi hizo pia zimebadilika. Hasa baada ya China kutekeleza sera ya Mageuzi na ufunguaji mlango mwishoni mwa miaka ya 70 ya karne iliyopita, uchumi wa China uliendelezwa haraka, bidhaa mbalimbali za kielektroniki zimeingia katika maisha ya kila siku ya wachina, na zimeleta urahisi kwa maisha ya watu na pia kuathiri mtindo wa jadi wa kusherehekea sikukuu.

     

    Siku ya kumkaribisha mungu wa utajiri

    Msikilizaji mpendwa, leo ni tarehe 23, pia ni tarehe 5 mwezi wa kwanza katika kalenda ya Kichina. Katika utamaduni wa China, siku ya tano baada ya kuingia katika mwaka mpya ni siku muhimu sana. Mambo makubwa yanayotakiwa kuzingatiwa ni pamoja na kumfukuza mungu wa umaskini, kumkaribisha mungu wa utajiri, na kufungua soko jipya. Inasemekana kwamba, watu hufungua milango na madirisha saa 6 kamili usiku wa manane siku hiyo, na kulipua fataki kwa imani kuwa, ukifanya hivyo, bila kujali utaelekea mashariki, magharibi, kusini, kaskazini au katikati, utapata utajiri mkubwa.

     

    Mila na desturi kuhusu vyakula wakati wa mwaka mpya wa jadi wa China

    Katika jamii ya Wachina, kuna mila na desturi mbalimbali kuhusu vyakula wakati wa kusherehekea sikukuu ya mwaka mpya, yaani sikukuu ya Spring. Na nyingi zinatokana na hadithi maelfu ya miaka iliyopita, na hadithi hizo zinapokezana na wachina wa kizazi baada ya kizazi. Wakati wa enzi ya Chunqiu, zaidi ya miaka 2,000 iliyopita, ofisa mwandamizi wa dola la Wu aitwaye Wu Zixu kabla ya kufariki aliwaambia wafuasi wake kuwa, "baada ya mimi kufariki, kama dola letu likikumbwa na taabu, na watu wetu wakikosa chakula, nendeni kwenye kuta za mlango wa Xiangmen na kuchimba chini futi tatu, mtaweza kupata chakula."

     

    Magulio ya hekalu

    "Miaohui" ni maneno ya Kichina. Tukitafsiri moja kwa moja neno la "miao", maana yake ni hekalu, na neno "hui" maana yake ni gulio. Magulio ya hekalu ni mila na desturi ya kidini ya kabila la Wahan nchini China. Yanahusu shughuli za kidini, na hufanyika karibu na mahekalu katika sikukuu za kidini au siku maalum, kama vile mwaka mpya wa jadi wa China. Hapo zamani, magulio ya hekalu yalishughulika na mambo ya kidini tu. Katika zama za kale, China ilikuwa na dini ya Kibudha na dini ya Kidao ambayo ni imani ya kienyeji.

     

    More>>
    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako