• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Ngoma ya Djembe yavutia mashabiki wengi China

    (GMT+08:00) 2015-02-12 11:45:23

    Katika kipindi cha leo, tutazungumzia ngoma za kiafrika nchini China. kama tunavyojua, katika lugha yetu ya Kiswahili ngoma ina maana mbili, moja ni ala ya kupiga, nyingine ni maonesho ya usanii, na zote hizo mbili zimependwa sana na watu wa China na kuvutia mashabiki wengi.

    Unaosikiliza sasa ni wimbo maarufu ya pop ya kichina unaoitwa Yi Shun Jian, au 'Ghafla' kwa kiswahili. Katika wimbo huo ala moja muhimu inayojitokeza masikioni ndiyo ni ngoma aina ya Djembe kutoka Afrika magharibi.

    Tangu ngoma hiyo ya Djembe iingie China mwaka 2008, mara moja midunde yake maalumu yenye uchangamfu imevutia mashabiki wengi. Kama ukitembelea kwenye sehemu nyingi za utalii hapa China, haswa zile zilizoko katika miji ya kale inayoendelezwa sasa kuwa vivutio vya utalii, kama vile mji wa kale wa Ping Yao mkaoni Shan'xi, kaskazini mwa China, mji wa kale wa Fenghuang mkoani Hunan, kusini mwa China au hata mji maarufu zaidi wa Lijiang mkoani Yunnan, kusini magharibi mwa China, huenda utashangaa kuona maduka ya ngoma za Djembe katika kila sehemu kati ya hizo, wenye duka hukaa ndani na kupiga ngoma pamoja na muziki. Midunde yake inasikika mbali sana mijini humo, na pia huvutia watazamaji wengi. Mbali na kuuza ngoma na kufanya maonesho ya ustadi wao, wenye duka hao pia wanatoa mafunzo ya kulipwa kwa watalii wanaotaka kujaribu kujifunza ala hiyo.

    Hapa Beijing, pia kuna kundi moja la mashabiki wa ngoma hiyo ya Djembe, kila Jumapili alasiri, wanakusanyika kwenye bustani ya ziwa Houhai, na kupiga ngoma kwa pamoja. Wachezaji hao hukaa kwenye duara, na ndani ya duara hiyo kuna kijana moja anayepiga ngoma akisimama. Kijana huyo mwenye umri wa miaka 30 hivi anaitwa Liu Yong, ni mwanzilishi na pia ni mkufunzi wa mashabiki hao wa ngoma. Hivi karibuni, tumepata fursa ya kuongea na Bw. Liu Yong.

    Mpaka sasa, kundi lake limeshirikisha mashabiki zaidi ya 300 mjini Beijing, na kila jumapili midunde ya ngoma zao imeongeza uchangamfu na kuwa mandhari maalumu katika bustani hiyo ya Houhai.

    Kwa kweli, ngoma ni ala isiyokosekana katika ngoma ya usanii wa kiafrika. Sasa basi tutupie macho ngoma ya usanii wa kiafrika hapa China. Kwa wachina wengi ambao hawajawahi kwenda Afrika, huona kuwa Afrika ni bara la mbali na lenye miujizi, wengi wao wana hamu ya kulitembelea bara hilo, na njia moja muhimu kwao kupata picha kuhusu Afrika ndiyo ni kupitia ngoma ya kiafrika yenye uchagamfu na furaha. Hapa kwenye mtaa wa Wangfujing, katikati ya jiji la Beijing, mwandishi wetu Ronald Mutie amekutana na kundi moja la ngoma ya kijadi ya Afrika linaloitwa Wamuchacha, anatuletea ripoti zaidi.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako