• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Pilikapiliya ya maandalizi ya mwaka mpya wa jadi wa China

    (GMT+08:00) 2015-02-12 15:01:51

    Alhamisi ijayo itakuwa ni siku ya mwaka mpya wa jadi wa China, kwa hiyo sasa maandalizi na shamrashamra za sikukuu hiyo vinaonekana, na jambo moja kubwa linalotokea katika kipindi kama hiki, yaani watu kusafiri, linaonekana sana. Kuwa nasi tukufahamishe nini kinaendelea kuanzia sasa hadi siku ya mkesha wa mwaka mpya wa jadi wa China.

    Pili: Tukianza na hilo ulilotaja la kusafiri, katika kipindi hiki kuelekea mwaka mpya wa jadi, wachina wengine sana wanasafiri kwenda maskani kwao. Kwanza ni wachina wanaishi kwenye mikoa mbalimbali wanarudi makwao kujumuika na familia zao kwa ajili ya sikukuu ya mwaka mpya wa jadi, wengine wanaoishi katika nchi za nje pia wanarudi China kujumuika na ndugu zao, na wengine wachache wanatumia muda huu kwenda kutalii ndani au nje ya China. Kwa hiyo kwa sasa kuna pilika nyingi za usafiri.

    Fadhili: Katika kipindi hiki naweza kusema mfumo wa usafiri wa umma wa China unakuwa na shinikizo sana. Lakini ni vizuri tukiwapa fursa kwa watanzania wenzetu ambao wamekuja hapa China, na kujionea hali ya usafiri ilivyo kuwa wakati wakija China. Pili umeongea nao, unasikia nini kutoka kwao?

    Pili: Kuna mmoja yeye alisema kwamba kikubwa ambacho alishangaa wakati alipo kwenye ndege, akakuta kwamba ndege nzima kuna wachina watupu, waafrika ni yeye na mwenzake na wengine wawili watatu. Baada ya kutafiti, akajua kwamba hiki ni kipindi cha sikukuu, kwa hiyo wachina wanatoka kule kurudi nyumbani na kusherehekea sikukuu ya mwaka mpya wa jadi wa China. Sasa hebu tumsikilize Bw. Mgimwa, yeye ndiye aliyeshuhudia kabisa tukio hilo.

    "Mimi nilikuja kwa mara ya kwanza, kwanza mimi mwenzangu Bw. Swai tulipokuwa tulikuja kwenye ndege, tulikuwa waafrika wawili tu, wengine wote ni wachina. Kila nilipouliza mwenzangu kwa nini sisi tulikuwa wachache. Akasema hawa wanakwenda kwenye sikukuu yao ya mwaka mpya, ambayo kwetu ni kubwa kama Krismas."

    Fadhili: kama tulivyosikia Bw. Mgimwa kwamba wachina wengi wanasafiri hata wale ambao wako nje, wanakuja kwa nchi yao. Na vilevile kwa mujibu ya makadirio ya mwaka huu, katika nchi hiyo yenye watu bilioni 1.3, idadi ya abiria , safari bilioni 2.8 zinakadiriwa kufanywa katika kipindi cha siku 40 za sikukuu ya mwaka mpya, hali ambayo ni sawa na kila mchina anasafiri mara mbili, yaani kwenda maskani halafu kurudi sehemu anakoishi.

    Pili: Nakumbuka rafiki mmoja mchina anayeishi Tanzania, aliponifahamisha safari hizo wakati wa mwaka mpya wa jadi wa China, alisema ni safari kubwa kuliko nyingine katika jamii ya binadamu, hali inayolingana na wanyama wa pori wanavyohama kila mwaka kati ya Serengeti na Masai Mara, ambazo ni safari kubwa zaidi katika jamii ya wanyama.

    Fadhili: Na imekadiriwa kuwa mwaka huu safari milioni 300 zitakuwa kwa njia ya reli, ni vigumu sana kununua tiketi za treni. Kwa hiyo vitendo vyovyote vinavyotibua utulivu wa usafiri wakati huu vinafuatiliwa sana.

    Pili:Kuanzia mwenzi Januari hadi sasa polisi wamekamata watu 2500 wanaofanya ujanja kwenye kununua tiketi na kuzilangua. Hawa jamaa ni wale wanaoiba data za vitambulisho vya watu na kutumia kununua tiketi, wenye vitambulisho wakienda kununua tiketi wanaambiwa tayari kumbukumbu zinaonesha wamenunua, kwani nchini China lazima tiketi ya treni itumiwe na mtu aliyenunua tiketi, yaani polisi anaweza kukagua kadi ya kitembulisho ya mnunuzi na data husika zinazohifadhiwa kwenye tiketi. Nakumbuka huko nyumba kulikuwa na tatizo la watu kusongamana kwenye vituo vya treni kununua tiketi, lakini sasa watu wanaweza kununua tiketi kwa njia ya internet au kuagiza kwa kupiga simu, kwa hiyo njia hizi mbali na kutatua tatizo kubwa zimetoa mwanya kwa baadhi ya watu kufanya uhalifu. Mhandisi wa usalama wa internet wa kampuni moja ya hapa Beijing Bw Li Tiejun anaeleza zaidi.

    "njia kubwa wanayotumia ni kuiba vitambulisho vya watu wengine na kusajili akaunti kadhaa, halafu wanatumia akaunti hizo kununua tiketi nyingi kadiri wawezavyo kabla wengine hawajanunua. Kwa kufanya hivi wanakuwa na tiketi nyingi za kulangua"

    Fadhili: Tukiangalia kwa undani kwenye hili la kusafiri, tunaweza kuona kitu kimoja ambacho ni msingi wa utamaduni wa China, familia na kujumuika kwa familia. Kwenye sikukuu labda watoto wanafurahia zaidi zawadi, chakula kitamu, na wengine wanafurahia mapumziko, lakini karibu wote wanafurahia zaidi kujumuika kwa familia. Hasa ukizingatia kwa mazingira ya sasa ya China baadhi ya wakati wanafamilia hawaoni kwa mwaka mzima, wanaona mara moja tu wakati wa sikukuu ya mwaka mpya.

    Pili: Kwa sasa watu wanaendelea kununua fataki, katika utamaduni wa China kuna imani kuwa kupiga fataki ni njia ya kuondoa pepo wabaya. Hii ni imani ambayo imekuwepo kwa maelfu ya miaka. Pamoja na kuwa wachina wanajua kabisa kuwa fataki ina hatari zake, kama vile watu kujeruhiwa, ajali za moto na hata kuchafua hewa, licha ya serikali kupiga marufuku baadhi ya maeneo kuwasha fataki, naona watu wanashindwa kuvumilia wanaendelea kuwasha fataki.

    Fadhili: Lakini uzuri ni kuwa serikali pia umeweka utaratibu mzuri zaidi, wa kutaka viwanda vya fataki kutengeneza fataki zisizosababisha uchafuzi mkubwa wa hewa, na hata maduka ya fataki pia yanatakiwa kuuza fataki zisizochafua hewa. Njia hii nadhani ina ufanisi zaidi katika kudhibiti tatizo hili, kwa kuwa kila serikali inapowataka watu wasiwashe fataki katika baadhi ya maeneo ya mji wao wanaendelea, kwa hiyo wale ambao hawatasikia hii njia itakuwa na ufanisi katika kulinda usafi wa hewa.

    Fadhili: Tunatakiwa kukumbuka kuwa wachina wana imani nyingine za jadi kuhusu mwaka mpya wa jadi. Kwa mfano huu mwaka tunaoingia ni mwaka wa mbuzi, na kwa maoni ya jadi hasa maoni ya wazee, mwaka wa mbuzi si mwaka mzuri. Kwa hiyo baadhi ya wanawake waja wazito hawataki kujifungua watoto katika mwaka wa mbuzi, na wengine wamefikia hata hatua ya kuwataka madaktari kuwasaidia wajifungue kabla ya tarehe 19 Februari yaani kabla ya mwaka wa mbuzi kuanza.

    Pili: Karibu kila jamii zinakuwa na imani fulani, lakini hizi imani kuna wakatu hazina msingi wa kisayansi, lakini zinafuatwa sana na watu. Mwaka huu wa kalenda ya kilimo ya China unaoisha yaani mwaka wa Farasi, wanawake wengi walijifungua watoto kwa kuwa wanaamini mwaka wa Farasi ni mwaka wa baraka, wanaamini watoto waliozaliwa mwaka huo wanakuwa na baraka. Sababu moja ni kuwa wanakwepa kupata watoto mwaka huu unaokuja.

    Fadhili: mfano mzuri ni dada mmoja wa mkoa wa Fujian mwenye umri wa miaka 28, huyu dada ni msomi kwa kuwa ana kazi nzuri, lakini ameamua kuahirisha kupata mtoto katika mwaka wa mbuzi kwa kuwa wazazi wake wamemwambia si mwaka mzuri kupata mtoto.

    "wazazi wangu wanafuata sana mila. Wamewataka baadhi ya ndugu zetu kuahirisha kupata watoto, kwa kuwa si vizuri kupata watoto katika mwaka wa mbuzi. Mwaka huu ni mbaya zaidi kwa kuwa majira ya Spring yameanza kabla ya sikukuu ya Spring, kwa hiyo wachina wanaona kuwa huu si mwaka kamili, nimeamua kuwa sitaki mtoto mwaka huu, kwa kuwa sitaki kuwapuuza wazazi wangu."

    Pili: Lakini vijana wa China kidogo wana maoni tofauti na wazee, wao hawaamini sana kuwa ukipata mtoto katika mwaka huu sio jambo zuri. Hata baadhi ya vijana wanadhani mwaka huu wa mbuzi ni kipindi kizuri cha kuzaa mtoto, kwani watoto hao watakabiliwa na ushindani mdogo kiasi katika kupata huduma ya matibatu, shule, ajira, n.k., kwani watoto wachache wanaozaliwa mwaka huu. Kwa hiyo kwenye miji mikubwa imani kama hizi hazina nguvu sana.

     

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako