• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Njia ya Hariri Baharini ya Karne ya 21 haitalisahau bara la Afrika

    (GMT+08:00) 2015-02-13 16:36:04

    Wakati nahodha wa kale wa China Zheng He alipoongoza msafara mkubwa wa wafanyabiashara katika safari ya kwanza ya biashara kupitia baharini wakati wa enzi ya Ming mwaka 1364-1644, alifanya mawasiliano kwa mara ya kwanza na mji wa bandari ambao baadaye ukawa mji wa Mombasa nchini Kenya. Zaidi ya miaka 600 baada ya Zheng kuweka njia ya mpango kamili kwa ajili ya Njia ya Hariri Baharini ya kisasa, biashara kati ya China na Kenya inaendelea. Fadhili Mpunji anaeleza zaidi katika ripoti ifuatayo

    Hivi sasa China inajenga reli ambayo itasaidia kurahisisha mawasiliano katika eneo hilo na kuendeleza zaidi njia iliyoanzishwa na Zheng kwa kuunganisha miji ya Mombasa na Nairobi nchini Kenya. Naibu mkurugenzi wa idara ya nchi za nje ya Kampuni ya Ujenzi na Mawasiliano ya China Zhang Baozhong amesema, ujenzi wa reli hiyo unaendelea vizuri na unatarajiwa kukamilika ndani ya miaka mitatu. Bw Zhang amesema, njia hiyo mpya ya reli itatoa nafasi 30,000 za ajira kwa wakazi wa Kenya, na itakuwa muhimu katika kuiunganisha Nairobi na njia ya hariri baharini, kwani itaunganisha mji huo na miji mikuu ya Uganda, Burundi, na Sudan Kusini. Ameongeza kuwa pindi mradi huo utakapokamilika, njia hiyo itasaidia kuunganisha eneo kubwa la Afrika Mashariki na bahari ya Hindi.

    Wakati China inawasilisha pendekezo la kufufua Njia ya Hariri Baharini ya Karne ya 21, mpango huu wa bara la Asia unapanuka hata nje ya Asia mpaka Afrika. Mbali na Mombasa, China pia inafadhili na kuendeleza bandari katika nchi mbalimbali za Afrika zikiwemo Djibouti, Tanzania, na Nigeria.

    Takwimu rasmi zinaonyesha kuwa, kwa mara ya kwanza mwaka jana thamani ya biashara ya pande mbili kati ya China na Afrika ilizidi dola bilioni 220 za kimarekani, na China sasa imekuwa mwenzi mkubwa wa biashara wa Afrika kwa miaka mitano mfululizo. Njia ya Hariri Baharini, kama ile ya nchi kavu, hivi sasa inaweka mkazo kwenye miradi ya ujenzi wa miundombinu. Ili kuiwezesha miradi hiyo, China imewekeza kwenye Benki ya Miundombinu ya Asia, ikiwa ni kando ya dola za kimarekani bilioni 40 ambazo imewekeza kwenye mfuko wa Njia ya Hariri.

    Ukanda wa kiuchumi wa Njia ya Hariri na Njia ya Hariri Baharini ya Karne ya 21 vinahusisha tamaduni mbalimbali na inachukua asilimia 63 ya idadi ya watu duniani. Tofauti ya tamaduni, desturi, sera na sheria, na mazingira ya kisiasa yanaweza kuwa ni vikwazo, lakini watu wengi wanaona kama hii ni fursa mpya kwa China na nchi za Afrika.

    Bw Bethwel Kinuthia, mchumi wa chuo kikuu cha Nairobi nchini Kenya anasemani wazi kuwa Njia ya Hariri Baharini imefungua njia kwa nchi za Afrika katika nyanja za soko jipya la bidhaa, uhamishaji wa teknolojia na ujuzi, pamoja na urahisi wa usafiri. Lakini mchumi huyo amesema, mara nyingi kuna matatizo katika usafirishaji wa bidhaa na huduma, ikiwa ni pamoja na miundombinu mibovu, gharama kubwa ya nishati, ambavyo vinapunguza uzalishaji, mabadiliko ya mara kwa mara ya hali ya hewa na ukosefu wa utulivu wa kisiasa. Amesema ni kwa kulinda hali tete ya mfumo wa mazingira ya asili, ndipo wafanyabiashara wa China na Afrika wanaweza kupunguza hatari na kuinua uwezo wao.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako