• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Unafiki wa Marekani kwenye mapambano dhidi ya ugaidi

    (GMT+08:00) 2015-02-17 19:04:54

    Rais Barack Obama atakutana na viongozi na maofisa waandamizi wa usalama kutoka nchi kadhaa kwenye mkutano utakaofanyika kesho mjini Washington, wenye lengo la kupambana na ugaidi unaoenea katika sehemu mbalimbali duniani. Mkutano huo utahudhuriwa na wataalam wa usalama pamoja na maofisa wa serikali za Uingereza, Canada, Australia, Ufaransa na Nigeria na nchi nyingine zilizokumbwa na mashambulizi ya kigaidi hivi karibuni zikiwemo.

    Ingawa Marekani inapenda kujidai kama kiongozi wa muungano wa kupambana na ugaidi, lakini uhusiano kati yake na makundi mengi ya msimamo mkali pamoja na watu wenye msimamo huo ni wenye utata na hata unatiliwa mashaka.

    Kati ya makundi mengi ya kigaidi duniani ambayo yamekuwa yakipata uungaji mkono kutoka serikali ya Marekani, kundi la Al Qaeda ni mfano mzuri wa kuonesha kwamba sera za mambo ya nje za Marekani zinatungwa kwa msingi wa kuangalia tu maslahi madogo ya muda mfupi.

    Tukiangalia historia, tutaona kuwa kati ya mwaka 1979 na mwaka 1989, ili kupambana na uvamizi wa Urusi dhidi ya Afghanistan, idara za ujasusi za Marekani ziliwahi kuunga mkono makundi mengi ya kiislamu yenye msimamo mkali nchini Afghanistan na katika nchi nyingine za kiislamu.

    Na baadaye, mfanyabiashara mmoja wa kiarabu aliibuka kuwa mfuasi mkubwa wa Idara ya Ujasusi ya Marekani CIA katika vita hiyo ambayo uhalisia wake ni kati ya Marekani ya Urusi, na jina la mfanyabiashara huyo ni Osama Bin Laden.

    Kundi la Al Qaeda, ambalo wafuasi wake wengi walipewa mafunzo na serikali ya Marekani limekuwa kundi kubwa na hatari zaidi la kigaidi duniani. Mikono ya kundi hilo imefika kwenye nchi karibu zote za kiislamu zilizotumbukia vitani.

    Tukiangalia kundi la Islamic State ambalo mienendo yake ni yenye msimamo mkali zaidi hata kwenye macho ya wapiganaji wa kawaida wa Al Qaeda, tutaona kuwa wafuasi wengi wakubwa wa IS walipewa mafunzo na CIA na makao makuu ya vikosi maalum vya Marekani katika kambi moja ya kisiri nchini Jordan mwaka 2012, taarifa ambayo imetolewa na maofisa wa Jordan.

    Zaidi ya hayo, alama za idara za ujasusi za Marekani zimefikia hata nje ya dunia ya kiislamu.

    Mnamo miaka ya 1990, vikosi maalum vya Marekani vilishirikiana na kundi la Los Pepes nchini Colombia kumwua mfanyabiashara mkubwa wa dawa za kulevya nchini humo Pablo Escobar. Baadaye baadhi ya viongozi wa kundi la Los Pepes walianzisha kundi linaloitwa vikosi vya umoja wa kujilinda vya Colombia ambalo linajulikana zaidi kama AUC. AUC ilihusika na mauaji mengi ya halaiki na mauaji dhidi ya wanasiasa nchini humo.

    Mnamo miaka ya 60 ya karne iliyopita, CIA pia ilitoa mafunzo na hifadhi kwa magaidi wawili waliojaribu kumwua kiongozi wa Cuba Fidel Castro na kupindua serikali yake.

    Wakati Marekani inapoinua kwa mara nyingine tena bendera ya kupambana na ugaidi, inatakiwa kuachana na ubinafsi wake na tabia yake ya kuangalia tu maslahi ya muda mfupi.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako