• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Mkutano Rais Silva Kirr na hasimu wake Riek Machar wakosa kufanyika

    (GMT+08:00) 2015-02-27 15:52:15

    Mkutano muhimu uliotarajiwa kati ya Rais wa Sudan Kusini na Kiongozi wa waasi Riek Machar, umegonga mwamba baada ya Kiir kuchelewa kufika mjini Addis Ababa, Ethiopia, ambako mpinzani wake Machar amewasili.

    Kutoonekana kwa Kiir kwenye mkutano huo kumegadhabisha Kitengo cha kulinda Usalama cha Umoja wa Mataifa ambacho kinatarajiwa kuiwekea serikali ya Sudan Kusini vikwazo vikali.

    Hayo yakiendelea, mjini Juba, Rais Salva Kiir ameamuru vikosi vyake vikomeshe mapigano na waasi na pia amewaita nyumbani wanasiasa kumi walioko uhamishoni na ambao aliwasamehe baada ya kudai kuwa walipanga njama za kuipindua serikali yake mwezi Desemba mwaka 2013.

    Kukiwa kumebaki siku saba ili Rais wa Sudan Kusini, Salva Kiir na kiongozi wa waasi Riek Machar waanzishe rasmi serikali ya mpito ya muungano wa kitaifa, wingu la kutatanisha lbado limetanda mjini Addis Ababa, Ethiopia, ambako wawili hao walitarajiwa kukutana kuweka sahihi kwenye makubaliano ya mwisho na ya amani ya kudumu.

    Wanadiplomasia wanaohudhuria mkutano huo wanaarifu kuwa wawakilishi hao wameshindwa kukubaliana kuunganisha vikosi vya serikali na vya waasi katika serikali ya muungano.

    IS: "Jihadi John", muaji wa mateka wa IS hatimaye ajulikana

    Hatimaye " jihadi John", mpiganaji wa kundi la wapigajai la IS ambaye alikua akionekana katika video nyingi za mauaji ya mateka, inasadikiwa kuwa anaitwa Mohammed Emwazi.

    " jihadi John" ni raia wa Uingereza mwenye asili ya Koweit, na anatambuliwa na idara za usalama, lakini ndugu zake ndio wamemtambua na kupelekea jarida la Washington Post kumfichua.

    Jihadi john amabye ssasa ametambuliwa kuwa ni Mohammed Emwazi alihusika kwa kuwakata vichwa mateka kutoka nchi za magharibi na wanajeshi wa Syria.

    Mohammed Emwazi, aliwasili nchini Uingereza akiwa na umri wa miaka sita, na alikua akiishi magharibi mwa London. Emwazi ni kutoka familia yenye maisha ya kati, na alihitimu chuo kikuu, na baadae aliufundisha katika shule mbalimbali kabla ya kuwa mwenye itikadi kali za kidini na baadae kujiunga na mwanaharakati anaeshirikiana na Al Shabab nchini Somalia. Mohammed Emwazi alijulikana na idara za usalama za Uingereza, ambazo zilimhoji mwaka 2006, baada ya kufukuzwa Tanzania. Idara ya ujasusi inasadikiwa kuwa ilijaribu kumsajili bila maafaniko, lakini mtu huyo alikua chini ya ulinzi mkali wa viongozi hadi alipopotea, na kushukiwa kuwa huenda alisafiri Syria.

    Bensouda awasili Uganda,kunani?

    Mwendesha mashtaka mkuu wa mahakama ya kimataifa kuhusu uhalifu wa kivita ICC Fatou Bensouda amewasili nchini Uganda ili kutafuta ushahidi kuhusu kesi ya aliyekuwa kamanda mkuu wa wapiganaji wa LRA nchini Uganda .

    Dominic Ongwen ambaye alisema alitekwanyara na LRA akiwa mtoto alifikishwa mbele ya mahakama ya ICC mjini Hague mnamo mwezi Januari akikabiliwa na mashtaka ya uhalifu wa kivita.

    Bensouda atazuru kazkazini mwa Uganda katika ziara ya siku tano ili kuzungumza na mashahidi mbali na kutembelea maeneo yaliotekelezewa uhalifu huo.

    Pia anatarajiwa kukutana na rais Yoweri Museveni wa Uganda ambaye amekuwa mkosoaji mkubwa wa mahakama hiyo ya ICC akiishtumu kwa kuwabagua viongozi wa Afrika.

    Uhusiano wa Marekani na Israel mashakani

    Hatua ya Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu ya kukosoa juhudi za kupata makubaliano juu ya mpango wa nyuklia wa Iran, kumezusha hisia kali na uharibifu wa ushirikiano katika mahusiano ya Israel na Marekani.

    Washirika hao wawili Marekani na Israel wanaendelea kutupiana maneno wakati ikiwa imesalia siku sita tu kabla ya waziri Mkuu Benjamin Netanyahu, kutoa hotuba yake katika bunge la Marekani wiki ijayo, akiangazia vitisho vya nyuklia kutoka Iran.

    Vuta nikuvute ilianza wakati Benjamin Netanyahu alipoyatuhumu mataifa yalio na nguvu duniani kwa kutelekeza ahadi ya kuizuwiya Iran kutengeneza silaha za nyuklia.

    Alisema Netanyahu kwamba anaheshimu ikulu ya Marekani na rais wa Marekani Barrack Obama lakini ni jukumu lake kufanya kila awezalo ili kuhakikisha usalama wa watu wa Israel.

    Hata hivyo Waziri wa mambo ya nchi za nje wa MarekaniJohn Kerry ambaye amehusika katika mazungumzo ya kimataifa na Iran juu ya mpango wake wa nyuklia amesema Netanyahu huenda akawa amekosea.

    Marekani yamteua balozi wake wa kwanza Somalia

    Wizara ya Mambo ya nje imetangaza kwamba Rais Barack Obama amemteua balozi wa Marekani nchini Somalia, ikiwa ni tukio la kihistoria kwani Marekani haikua na mwakilishi Mogadidiscio tangu mwaka 1991.

    Rais Obama amemteua Katherine Dhunani, ambaye alikua akisimamia ubalozi mdogo katika mji wa Hyderabad, nchini India, kuwa balozi wa Marekani nchini Somalia.

    Hyderabad ataendesha shughuli zake wakati huu, akiwa katika mji mkuu wa Kenya, Nairobi. Uamzi huu ni kutokana na hali ya usalama katika mji wa Mogadishu ambayo haijaimarika.

    200 wauwawa na maporomoko ya theluji

    Zaidi ya watu 200 wameuawa katika mfululizo wa maporomoko ya theluji katikamaeneo mbali mbali nchini Afghanistan, huku ikihofiwa kwamba vifo vinaweza kuongezeka.

    Kwa mujibu wa kaimu wa mkoa Abdul Rahman Kabiri maeneo yalioripotiwa vifo vingi ni katika jimbo la Panjshir, kaskazini mwa mji mkui ya Kabul, ambapo angalau 168 watu waliuawa.

    Maporomoko hayo yalitokea baada ya siku ya theluji nzito, na kuharibiwa nyumba zaidi ya 100 katika mkoa huku ikifunga pia barabara kuu, na kuifanya vigumu kwa wafanyakazi wa kuwaokoa kufikia vijiji.

    Kwingineko, watu 18 walikufa katika kijijini cha kaskazini mashariki mwa jimbo la Badakhshan na 12 katika mkoa wa Nuristan kaskazini.

    Mazishi kwa waathirika yailianza Alhamisi katika kijiji Panjshir huku nazo Helikopta mbili zikiendelea kuleta misaada kwa waanga.

    Maporomoko ya theluji ni ya kawaida katika maeneo ya Afghanistan ya milima katika majira ya baridi.

    Mwaka 2010, zaidi ya watu 165 walifariki katika maporomoko kwenye eneo la Salang Pass na mwaka wa 2012 tukio linguine kama hilo likawauwa watu 145.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako