• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Marekani na EAC zasaini makubaliano ya ushirikiano wa kibiashara

    (GMT+08:00) 2015-02-27 17:34:45

    Marekani itatoa msaaada wa kiteknolojia kwa nchi za Jumuiya ya Afrika mashariki EAC ili kuzisaidia kupunguza vizuizi vya kibiashara na kuongeza ushindani wa kibiashara.

    Hayo yamo kwenye makubaliano yaliyosainiwa jana na mwakilishi wa biashara wa Marekani Michael Froman na mawaziri wa biashara wa nchi wanachama wa EAC. Makubaliano hayo yatajenga uwezo katika maeneo makuu matatu, yaani urahisishaji wa biashara, hatua za ulinzi wa afya na kudhibiti magonjwa kwa mimea, na vizuizi vya kiteknolojia kwa biashara. Bw. Michael Froman amesema, makubaliano hayo ni tukio muhimu kwa mpango unaojulikana kama "Trade Africa" uliotolewa na serikali ya rais Barack Obama, na yatahimiza mafungamano ya uchumi wa nchi za EAC na kuimarisha uhusiano wa kiuchumi na kibiashara kati ya Marekani na EAC.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako