• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • China yasema jumuiya ya kimataifa ina maoni sahihi juu ya mahali linapotoka tishio dhidi ya mtandao wa internet wa kimataifa

    (GMT+08:00) 2015-02-27 19:49:06

    Msemaji wa wizara ya mambo ya nje ya China Hong Lei amesema, China inapinga udukuzi katika mtandao wa internet, na jumuiya ya kimataifa inapaswa kushirikiana kukabiliana na suala hili ili kulinda amani, usalama, uwazi na ushirikiano katika mtandao wa internet.

    Hong Lei amesema hayo kufuatia ripoti iliyotolewa hivi karibuni na ofisi ya Mkurugenzi wa Ujasusi nchini Marekani inayodai kuwa China ni moja ya nchi zinazotishia usalama wa mtandao wa Internet. Amesema baada ya kufichuliwa kwa upelelezi mkubwa uliofanywa na Marekani kwa nchi nyingine kwenye mtandao wa internet, jumuiya ya kimataifa ina maoni sahihi kuhusu mahali linapotoka tishio dhidi ya mtandao wa internet wa kimataifa. Ameongeza kuwa, China sio tu ni mlinzi thabiti wa amani wa utulivu wa mtandao wa internet wa kimataifa, bali pia ni mtetezi wa kujenga utaratibu kwenye mtandao huo.

    Mwezi uliopita, China na nchi nyingine wanachama wa Jumuiya ya Ushirikiano ya Shanghai ziliwasilisha mswada wa marekebisho wa "kanuni za kimataifa za mwenendo kwa usalama wa taarifa" kwenye Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa, na kutoa mapendekezo zaidi ya kulinda usalama wa mtandao wa internet.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako