• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • China kuorodhesha majina ya maofisa wanaoingilia utendaji wa mahakama

    (GMT+08:00) 2015-02-27 19:53:22

    China itaanza kuorodhesha na kutoa adhabu kali kwa maofisa wanaoingilia utendaji wa sheria chini ya mpango uliopitishwa na kamati ya juu ya mpango wa mageuzi.

    Taarifa iliyotolewa na Kikundi cha uongozi wa mageuzi ya pande zote baada ya mkutano wake imesema, utaratibu huo mpya utatumika kama kinga itakayolinda uhuru wa idara za kisheria, na unaunda mchakato mpana wa mageuzi ya kisheria yaliyofikiwa katika mkutano wa kamati kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China uliofanyika mwezi Oktoba mwaka jana.

    Taarifa hiyo imesema, maofisa wa chama na serikali wana wajibu mkubwa wa kutimiza utawala wa sheria nchini China, na wanatakiwa wajizuie kuingilia upelelezi na usikilizaji wa kesi.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako