• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Wapiganaji 5, 000 wa kigeni wapo nchini Libya

    (GMT+08:00) 2015-02-28 19:14:15

    Waziri wa mambo ya kigeni wa Libya Bw Mohamed al-Dairi amesema kuna wapiganaji 5, 000 wa kigeni nchini humo na kutoa wito wa msaada wa kimataifa katika kupambana na ugaidi.

    Waziri huyo amenukuliwa akisema kiongozi wa kundi la kigaidi la Emir ambalo lina uhusiano na lile la Islamic State nchini Libya lililohusika na mashambulizi ya mabomu mjini al-Gubba ni raia wa Yemeni.

    Al-Dairi pia ametoa wito kwa jumuiya ya kimataifa kutoa silaha kwa jeshi la Libya akisistiza kuwa tishio la kigaidi sio tu ni kwa Libya bali pia eneo lote la kaskazini mwa Afrika na bara Ulaya.

    Mipaka ya Libya isiokuwa na doria kali imewezesha wapiganaji kuingia nchini humo wakitokea Nigeria, Mali na Niger.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako