• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Wapiganaji 8 wa al-shabab wauawa na vikosi vya pamoja nchini Somalia

    (GMT+08:00) 2015-02-28 19:14:33

    Wapiganaji wanane wa kundi la al-shabab wameuawa baada ya kushambuliwa na vikosi vya serikali vikisaidiwa na vya Umoja wa Afrika katika jimbo la Bakool kusini magharibi ya Somalia. Akizungumza na waandishi wa habari, kamanda wa jeshi la Somalia Bw Abdirahman Mohammed amesema oparesheni hiyo ya pamoja iliyodumu kwa saa 10 ilifanyika katika mji wa Celbaar. Mohamed amesema wanajeshi watatu wameuawa na wengine 15 kujeruhiwa kwenye mapambano hayo. Hata hivyo kundi la al-Shabab limetangaza kuwauawa zaidi ya wanajeshi 10 wa serikali na kusisitiza kuwa bado wanaudhibiti mji huo. Wakati huo huo afisa wa serikali ya Somalia amesema vikosi vya serikali tayari vimerudi kwenye kambi yao baada ya shambulizi hilo. Vikosi vya Somalia vikisaidiwa na vya Umoja wa Afrika vimepata mafanikio makubwa katika mwaka mmoja uliopita kwa kunyakua miji mikubwa kutoka kwa wapiganaji wa al-Shabab.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako